عَن سَهْلِ بْنِ حُنَيْفٍ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَنْ سَأَلَ اللهَ الشَّهَادَةَ بِصِدْقٍ بَلَّغَهُ اللهُ مَنَازِلَ الشُّهَدَاءِ، وَإِنْ مَاتَ عَلَى فِرَاشِهِ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 1909]
المزيــد ...
Kutoka kwa Sahali bin Hunaif radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Atakayemuomba Mwenyezi Mungu shahada (yaani kufa shahidi) kwa dhati, basi atamfikisha daraja ya mashahidi hata kama atafia juu ya godoro lake"
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 1909]
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayeomba shahada na kuuawa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na akawa mkweli na mwenye ikhlasi katika nia yake hiyo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi Mwenyezi Mungu atamjaalia kupata daraja za mashahidi kwa nia yake ya kweli, hata akifa kitandani katika hali isiyokuwa jihadi.