عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَا يَزَالُ البَلاَءُ بِالمُؤْمِنِ وَالمُؤْمِنَةِ فِي نَفْسِهِ وَوَلَدِهِ وَمَالِهِ حَتَّى يَلْقَى اللَّهَ وَمَا عَلَيْهِ خَطِيئَةٌ».
[حسن] - [رواه الترمذي وأحمد] - [سنن الترمذي: 2399]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Majaribio hayaachi kumpata muumini wa kiume na muumini wa kike katika nafsi yake, na watoto wake, na mali yake mpaka atakapokutana na Mwenyezi Mungu ilhali hana dhambi hata moja."
[Ni nzuri] - - [سنن الترمذي - 2399]
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa: “Balaa na mtihani havikomi kwa muumini wa kiume na wa kike, katika afya yake na mwili wake, na kwa watoto wake, kama magonjwa, kifo, uasi na mengineyo, na katika mali yake kutiwa umasikini, kutoweka kwa biashara, kuibiwa, kuvurugika kwa maisha na dhiki katika riziki, na ugumu wa maisha, mpaka Mwenyezi Mungu atamfutia dhambi zake zote kwa mateso haya, ili atakapokutana na Mwenyezi Mungu atakuwa kasafishika na madhambi na maovu yote aliyoyafanya.