+ -

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بنِ عُمرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«كُلُّكُمْ رَاعٍ فَمَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ، فَالأَمِيرُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْهُمْ، وَالرَّجُلُ رَاعٍ عَلَى أَهْلِ بَيْتِهِ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْهُمْ، وَالمَرْأَةُ رَاعِيَةٌ عَلَى بَيْتِ بَعْلِهَا وَوَلَدِهِ وَهِيَ مَسْئُولَةٌ عَنْهُمْ، وَالعَبْدُ رَاعٍ عَلَى مَالِ سَيِّدِهِ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْهُ، أَلاَ فَكُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 2554]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdillah Bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yao: Yakwamba Mtume -Rehema na amani za Allah ziwe juu yake- amesema:
"Kila mmoja miongoni mwenu ni mchunga hivyo ataulizwa kuhusu raia wake, kiongozi anayewaongoza watu ni mchunga naye ndiye atakayeulizwa kuhusu wao, na mwanaume ni mchunga kwa watu wa nyumbani kwake naye ndiye wa kuulizwa kuhusu wao, na mwanamke ni mchunga katika nyumba ya mumewe na watoto wake naye ndiye atakayeulizwa kuhusu wao, na mja ni mchunga juu ya mali ya bosi wake, naye ndiye atakayeulizwa juu ya mali hiyo, tambueni kuwa kila mmoja kati yenu ni mchunga na kila mmoja ataulizwa kuhusu raia wake".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 2554]

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume rehema na amani zimfikie kuwa kila muislamu katika jamii anamajukumu anayoyasimamia na anayoyabeba, Imamu na kiongozi ni mchunga katika majukumu aliyopewa na Allah kuyasimamia, anatakiwa kuhifadhi sheria zao, na kuwalinda dhidi ya mwenye kuwafanyia uadui, na kumpiga vita adui yao, na kutopoteza haki zao, Na mwanaume kwa watu wa nyumba yake amelazimishwa kuwasimamia kwa matumizi, na kuishi nao vizuri, na kuwasomesha na kuwaadabisha, Na mwanamke katika nyumba ya mumewe ni mchunga kwa kuipangilia vizuri nyumba yake, na kuwalea watoto wake, naye ataulizwa kuhusu hilo, Na mfanyakazi mmilikiwa na mwajiriwa ataulizwa katika mali ya bosi wake kwa kusimamia kuhifadhi kile kilicho mkononi mwake, na huduma zake, naye ataulizwa kuhusu hilo, kila mmoja ni mchunga katika vile alivyopewa kuvichunga, na kila mmoja ataulizwa kuhusu raia wake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف الأوكرانية الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Majukumu katika jamii ya kiislamu ni ya watu wote, na kila mmoja ni kulingana na nafasi yake na uwezo wake na majukumu yake.
  2. Ukubwa wa majukumu ya mwanamke, na hii ni kwa kusimamia haki za nyumba ya mume wake na majukumu yake kwa watoto wake.