+ -

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ رضي الله عنهما أنَّ رَسولَ اللَّهِ صلَّى اللَّهُ عليْه وسلَّمَ، قال:
«قَدْ أَفْلَحَ مَن أَسْلَمَ، وَرُزِقَ كَفَافًا، وَقَنَّعَهُ اللَّهُ بما آتَاهُ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 1054]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abdallah Ibn Amri -radhi za Allah ziwe juu yao wawili ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amesema:
"Hakika amefaulu aliye jisalimisha, na akaruzukiwa kujizuia na kuombaomba, na Allah akamkinaisha kwa kile alichompa".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 1054]

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba amefaulu na amebahatika atakayemtii Mola wake akaongozwa na akawezeshwa kuingia katika Uislamu, na akaruzukiwa katika halali kiasi cha mahitaji yake pasina ziada wala mapungufu, na Mwenyezi Mungu akamjaalia kukinai na kuridhika na kile alichompa.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kiassam الأمهرية الهولندية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Utukufu wa mtu upo katika ukamilifu wa dini yake na kupata cha kumtosheleza katika maisha yake na kutosheka kwake na kile alichopewa na Mwenyezi Mungu.
  2. Himizo la kutosheka kwa kile ulichopewa katika dunia ikiwa ni pamoja na Uislamu na sunna.