عَنْ إِيَاسِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي ذُبَابٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«لَا تَضْرِبُوا إِمَاءَ اللَّهِ» فَجَاءَ عُمَرُ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: ذَئِرْنَ النِّسَاءُ عَلَى أَزْوَاجِهِنَّ، فَرَخَّصَ فِي ضَرْبِهِنَّ، فَأَطَافَ بِآلِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نِسَاءٌ كَثِيرٌ يَشْكُونَ أَزْوَاجَهُنَّ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَقَدْ طَافَ بِآلِ مُحَمَّدٍ نِسَاءٌ كَثِيرٌ يَشْكُونَ أَزْوَاجَهُنَّ، لَيْسَ أُولَئِكَ بِخِيَارِكُمْ».
[صحيح] - [رواه أبو داود وابن ماجه] - [سنن أبي داود: 2146]
المزيــد ...
Kutoka kwa Jabiri bin Abdillah -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Msiwapige vijakazi wa Mwenyezi Mungu" Akaja Omari kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Hivi sasa wanawake wamepata ujasiri kwa waume zao, basi akaruhusu kuwapiga, baada ya muda wakaanza kuzunguka katika familia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake wanawake wengi wakiwashitakia waume zao, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika wamekuja katika familia za Muhammad wanawake wengi wakiwashitakia waume zao, (wanaume) hao si bora kati yenu".
[Sahihi] - - [سنن أبي داود - 2146]
Alikataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwapiga wanawake, akaja kiongozi wa Waumini Omari bin Khattwabi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wanawake wamepata ujasiri kwa waume zao, na wamekuwa na tabia mbovu. Akaruhusu rehema na amani ziwe juu yake kuwapiga kipigo kisichojeruhi inapopatikana sababu ya hilo, kama kukataa kwao kutimiza wajibu wao kwa waume zao na kuwaasi, na mfano wa hayo. Baada ya hapo wakaja wanawake kwa wake wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakishitakia kupigwa na waume zao kipigo chenye kujeruhi, na matumizi mabaya ya ruhusa hii, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Wanaume hao, wanaowapiga wake zao kipigo chenye kujeruhi, si watu bora kwenu.