عن أسامة بن زيد رضي الله عنهما عن النبي صلى الله عليه وسلم قال:
«مَا تَرَكْتُ بَعْدِي فِتْنَةً أَضَرَّ عَلَى الرِّجَالِ مِنَ النِّسَاءِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 5096]
المزيــد ...
Kutoka kwa Osama bin Zaidi -Radhi za Allah ziwe juu yao- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Sikuacha baada yangu fitina yenye madhara zaidi kwa wanaume kuliko wanawake".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 5096]
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuacha baada yake majaribu na mtihani wenye madhara makubwa kwa wanaume kuliko wanawake; Mwanamke akiwa ni katika familia yake huenda mume akamfuata mwanamke katika kwenda kinyume na sheria, na akiwa ni mwanamke wa kando yaweza kuwa ni kwa sababu ya kuchanganyika naye na kukaa naye faragha, na maovu mengine yanayoweza kusababishwa na hilo.