عَنْ ابْنِ عُمَرَ رَضيَ اللهُ عنهُما أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَا حَقُّ امْرِئٍ مُسْلِمٍ لَهُ شَيْءٌ يُوصِي فِيهِ، يَبِيتُ ثَلَاثَ لَيَالٍ، إِلَّا وَوَصِيَّتُهُ عِنْدَهُ مَكْتُوبَةٌ»، قَالَ عَبْدُ اللهِ بْنُ عُمَرَ رضي الله عنهما: «مَا مَرَّتْ عَلَيَّ لَيْلَةٌ مُنْذُ سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ذَلِكَ إِلَّا وَعِنْدِي وَصِيَّتِي».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 1627]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa bin Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Hakuna haki yoyote ya mtu muislamu anayotakiwa kuitolea usia, isipokuwa ahakikishae halali siku tatu, isipokuwa usia wake uwe umeandikwa kwake", akasema Abdallah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao: "Haukuwahi kupita usiku mmoja tangu nilipomsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akilisema hilo isipokuwa usia wangu nilikuwa nao".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 1627]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuwa haitakiwi kwa muislamu anapokuwa na kitu cha kutolea usia katika haki au mali hata kama ni ndogo, alale siku tatu, isipokuwa ahakikishe usia wake umeandikwa kwake. Akasema Abdallah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao: Sikuwahi kulala hata usiku mmoja tangu nilipomsikia rehema na amani ziwe juu yake akilisema hilo isipokuwa nilikuwa nikikaa na usia wangu.