+ -

عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ مِحْصَنٍ الْأَنْصَارِيِّ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَنْ أَصْبَحَ مِنْكُمْ مُعَافى فِي جَسَدِهِ، آمِنًا فِي سِرْبِهِ، عِنْدَهُ قُوتُ يَوْمِهِ، فَكَأَنَّمَا حِيزَتْ لَهُ الدُّنْيَا».

[حسن] - [رواه الترمذي وابن ماجه] - [سنن ابن ماجه: 4141]
المزيــد ...

Kutoka kwa Ubaidillaah bin Mihswan Al-Answari radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Atakayeamka miongoni mwenu akiwa na afya njema katika mwili wake, akiwa na amani katika mji wake, na anamiliki chakula cha siku yake hiyo, basi atakuwa ni kama kakusanyiwa dunia (yote)".

[Ni nzuri] - - [سنن ابن ماجه - 4141]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba atakayeamka miongoni mwenu enyi waislamu akiwa mzima wa afya katika mwili wake akiwa amesalimika na matatizo na magonjwa, akiwa na amani ndani ya nafsi yake na watu wake na familia yake na barabara zake, na akiwa hana hofu, na akiwa na chakula cha halali cha kumtosha kwa siku yake; basi ni kana kwamba kakabidhiwa dunia yote nzima.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kiassam الهولندية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa haja ya mtu kuwa na afya na amani na nguvu.
  2. Ni wajibu kwa mja amhimidi Mwenyezi Mungu Mtukufu na amshukuru kwa neema hizi.
  3. Himizo la kuridhika na kuipa nyongo dunia.