عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللهِ رضي الله عنهما أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«اتَّقُوا الظُّلْمَ، فَإِنَّ الظُّلْمَ ظُلُمَاتٌ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، وَاتَّقُوا الشُّحَّ، فَإِنَّ الشُّحَّ أَهْلَكَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ، حَمَلَهُمْ عَلَى أَنْ سَفَكُوا دِمَاءَهُمْ وَاسْتَحَلُّوا مَحَارِمَهُمْ».

[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Na kutoka kwa Jaabir Bin Abdillah -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-
"Ogopeni dhulma, kwa hakika dhulma ni giza siku ya kiyama. Na ogopeni tamaa, kwa hakika tamaa iliwaangamiza walio kuwepo kabla yenu. Iliwapelekea kumwaga damu zao, na kuhalalisha yaliyo haramu kwao".

Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Alitahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu dhulma, ikiwemo: Kuwadhulumu watu na kujidhulumu mwenyewe na kufanya dhulma katika haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, nayo kuacha kumpa kila mwenye haki haki yake, nakuwa dhulma ni giza kwa wafanyaji dhulma siku ya Kiyama ikiwemo kupata matatizo na misukosuko, Na akakataza tamaa ambayo ni ubahili uliopitiliza pamoja na pupa, na ikiwemo kufanya uzembe katika kutekeleza haki ya mali na tamaa iliyopitiliza ya kuipupia dunia, Na aina hii ya dhulma iliwaangamiza Umma waliokuwa kabla yetu, kiasi ambacho iliwapelekea kuuana wao kwa wao, na kuyahalalisha yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu katika mambo yaliyoharamishwa.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kutoa mali na kuwaliwaza ndugu ni katika sababu za kupendana na kuwa na mawasiliano.
  2. Ubahili na tamaa huwavuta watu katika maasi na machafu na madhambi.
  3. Kuchukua mazingatio kupitia hali za wale waliotangulia.