عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ:
«بَيْنَمَا جِبْرِيلُ قَاعِدٌ عِنْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سَمِعَ نَقِيضًا مِنْ فَوْقِهِ، فَرَفَعَ رَأْسَهُ، فَقَالَ: هَذَا بَابٌ مِنَ السَّمَاءِ فُتِحَ الْيَوْمَ لَمْ يُفْتَحْ قَطُّ إِلَّا الْيَوْمَ، فَنَزَلَ مِنْهُ مَلَكٌ، فَقَالَ: هَذَا مَلَكٌ نَزَلَ إِلَى الْأَرْضِ لَمْ يَنْزِلْ قَطُّ إِلَّا الْيَوْمَ، فَسَلَّمَ، وَقَالَ: أَبْشِرْ بِنُورَيْنِ أُوتِيتَهُمَا لَمْ يُؤْتَهُمَا نَبِيٌّ قَبْلَكَ: فَاتِحَةُ الْكِتَابِ، وَخَوَاتِيمُ سُورَةِ الْبَقَرَةِ، لَنْ تَقْرَأَ بِحَرْفٍ مِنْهُمَا إِلَّا أُعْطِيتَهُ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 806]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema:
"Pindi Jibrili alipokuwa amekaa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisikia kishindo kutoka juu yake, akanyanyua kichwa chake, akasema: "Huu ni mlango kutoka Mbinguni umefunguliwa leo haukuwahi kufunguliwa kabisa isipokuwa leo, kisha akateremka kutoka kwenye mlango ule Malaika, akasema: "Huyu ni Malaika ameteremka Ardhini hakupata kuteremka kabisa isipokuwa leo, akawasalimia, kisha akasema: "Pokea habari njema ya kupewa Nuru mbili hakupewa Nabii yeyote kabla yako: Ufunguzi wa kitabu (Alfatiha) na Aya za mwisho katika Suratul-baqarah, hautasoma herufi miongoni mwa Sura hizo mbili isipokuwa utapewa (unacho hitaji)"
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 806]
Malaika Jibril amani iwe juu yake alikuwa amekaa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasikia sauti kutoka mbinguni kama sauti ya mlango unapofunguliwa, Jibril akanyanyua kichwa chake na macho yake mbinguni, kisha akaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba mlango huu kutoka mbinguni umefunguliwa leo, na haukuwahi kufunguliwa katu isipokuwa leo, akateremka kutoka humo Malaika kuja Ardhini, hakuwahi kuteremka kabla isipokuwa leo, Malaika akamtolea salamu Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akasema kumwambia: Kuwa na habari njema ya kupata Nuru mbili ulizopewa, ambazo hakuwahi kupewa Nabii yeyote kabla yako; nazo ni: Suratul-Fatiha, na Aya mbili za mwisho wa suratul-Baqara. Kisha Malaika akasema: Hatosoma yeyote harufi moja katika hizo isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa yale yaliyomo ndani yake miongoni mwa heri na dua na maombi.