عن أنس بن مالك رضي الله عنه:
أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ لَا يَرُدُّ الطِّيبَ.

[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 2582]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-:
Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa hakatai marashi.

[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [Swahiih Al Bukhaariy - 2582]

Ufafanuzi

Ilikuwa katika muongozo wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa hakatai marashi na anayapokea; kwa sababu ni mepesi kubebeka na yana harufu nzuri.

Katika Faida za Hadithi

  1. Inapendeza kukubali zawadi ya marashi; kwa sababu hakuna tabu kuyabeba kwake na wala hakuna masimango ikiwa mtu atayakubali.
  2. Ukamilifu na tabia njema za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa kutokataa marashi, na kukubali zawadi ya yeyote mwenye kumzawadia.
  3. Himizo la kutumia marashi.
Kuonyesha Tarjama
Lugha: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Ziada (63)