عن أبي مسعود رضي الله عنه قال: قال النبي صلى الله عليه وسلم:
«مَنْ قَرَأَ بِالْآيَتَيْنِ مِنْ آخِرِ سُورَةِ الْبَقَرَةِ فِي لَيْلَةٍ كَفَتَاهُ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 5009]
المزيــد ...
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Atakayesoma aya mbili za mwisho wa suratul Baqara zitamtosheleza".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 5009]
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayesoma aya mbili za mwisho katika suratul-Baqara usiku, basi Mwenyezi Mungu atamtosheleza na shari na kila lenye kuchukiza, na imesemwa: Zitamtosheleza na kisimamo cha usiku, na imesemwa: Zita mtosha na nyiradi zote, na imesemwa kuwa: Ni kiwango kidogo kinachoweza kumtosheleza mtu na kusoma Qur'ani katika kisimamo cha usiku, na imesemwa kinyume na hivyo, na huenda yote yaliyotajwa yanakusanywa na tamko hilo.