عن ابن مسعود رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «مَنْ قَرَأ حَرْفاً مِنْ كِتاب الله فَلَهُ حَسَنَة، والحَسَنَة بِعَشْرِ أمْثَالِها، لا أقول: ألم حَرفٌ، ولكِنْ: ألِفٌ حَرْفٌ، ولاَمٌ حَرْفٌ، ومِيمٌ حَرْفٌ».
[صحيح] - [رواه الترمذي]
المزيــد ...

Kutoka kwa Bin Mas'udi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake: "Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu basi atapata jema moja na jema hilo kwa mema kumi mfano wake, sisemi: AlifLamMim kuwa ni herufi moja, lakini: Alif ni herufi, na Lam ni herufi, na Mim ni herufi".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy

Ufafanuzi

Anapokea bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- katika hadithi hii kuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake ameeleza kuwa kila muislamu anayesoma herufi moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu basi malipo yake kwa herufi moja ni mema kumi, na kauli yake: "Sisemi Alif Lam Mim ni herufi" Yaani: sisemi mkusanyiko wa herufi hizi tatu kuwa ni herufi moja, bali Alif ni herufi na Lam ni herufi na Mim ni herufi, atalipwa msomaji wa herufi hizo mema thelathini, hii ni neema kubwa na ni malipo makubwa, hivyo ni lazima kwa mwanadamu azidishe kukisoma kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuhimizwa juu ya kusoma Qur'ani.
  2. Nikuwa kwa msomaji kwa kila herufi katika kila neno analolisoma ana jema linalozidishwa.
  3. Kubainishwa maana ya herufi, na kutofautishwa kati yake na neno.
  4. Upana wa rehema za Mwenyezi Mungu na ukarimu wake, kiasi kwamba amewazidishia waja malipo kwa fadhila na ukarimu toka kwake.
  5. Kuthibitisha kuwa maneno ya Mwenyezi Mungu ni kwa sauti na herufi.