+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ:
عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «قَالَ اللَّهُ: كَذَّبَنِي ابْنُ آدَمَ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ ذَلِكَ، وَشَتَمَنِي وَلَمْ يَكُنْ لَهُ ذَلِكَ، فَأَمَّا تَكْذِيبُهُ إِيَّايَ فَقَوْلُهُ: لَنْ يُعِيدَنِي، كَمَا بَدَأَنِي، وَلَيْسَ أَوَّلُ الخَلْقِ بِأَهْوَنَ عَلَيَّ مِنْ إِعَادَتِهِ، وَأَمَّا شَتْمُهُ إِيَّايَ فَقَوْلُهُ: اتَّخَذَ اللَّهُ وَلَدًا وَأَنَا الأَحَدُ الصَّمَدُ، لَمْ أَلِدْ وَلَمْ أُولَدْ، وَلَمْ يَكُنْ لِي كُفْؤًا أَحَدٌ».

[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 4974]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-:
Kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Amesema Mwenyezi Mungu: kanipinga mwanadamu na hakustahiki kufanya hivyo, na amenitukana na hakustahiki kufanya hivyo, na ama kunipinga kwake ni kauli yake: Mwenyezi Mungu hatonirudisha kuwa hai, kama alivyonianzisha, na si kuanza kuumba ni kwepesi zaidi kwangu kuliko kurudisha, na kunitukana kwake ni kauli yake: kuwa Mwenyezi Mungu kajifanyia mwana, na mimi ndiye mmoja mwenye kukusudiwa, sikuzaa wala sikuzaliwa, na wala hakuna anayefanana nami hata mmoja".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 4974]

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika hadithil Qudsi yakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ameeleza kuhusu washirikina na makafiri kuwa wao humkanusha na humsifu kwa sifa za mapungufu na za aibu, na hawakutakiwa kufanya hivyo.
Ama kumkanusha kwao Mwenyezi Mungu: Ni kudai kwao kuwa Mwenyezi Mungu hatowarejesha kwa mara nyingine baada ya kufa kwao kama alivyowaumba mara ya kwanza kutoka katika kutokuwepo, akawajibu kuwa aliyeanza kuumba mwanzo anauwezo wa kuwarudisha, bali hilo ni jepesi mno, japo kuwa uhalisia kwa Mwenyezi Mungu yote ni mepesi, kuumba kwanzia mwanzo na kurudisha, kwani Mwenyezi Mungu juu ya kila kitu ni muweza.
Na ama kutukana kwao: Ni kauli yao: Kuwa yeye ana mtoto, akawajibu kuwa yeye ni wa pekee aliyepwekeka kwa ukamilifu wote katika majina yake na sifa zake na vitendo vyake, aliyetakasika na kila mapungufu na aibu, wa pekee asiyehitaji kwa yeyote, na anahitaji kwake kila mmoja, na hakuwahi kuwa mzazi wa yeyote, na hakuwahi kuwa mtoto wa yeyote, na hakuna yeyote anayefanana naye hata mmoja kwa kuwa na mfanano au mwendano, ametakasika na kutukuka.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف الأوكرانية الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuthibitisha ukamilifu wa uweza wa Mwenyezi Mungu.
  2. Kumethibitishwa kufufuliwa baada ya kifo.
  3. Kukufuru mwenye kupinga kufufuliwa au akamnasibishia mtoto Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  4. Mwenyezi Mungu Mtukufu hana mfano wala mwenye kufanana naye.
  5. Upana wa upole wa Mwenyezi Mungu, na kuwapa kwake muda makafiri huenda wakatubia na kurejea.
Ziada