عَن عَبْدِ اللهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ رضي الله عنهما أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ:
«إِنَّ قُلُوبَ بَنِي آدَمَ كُلَّهَا بَيْنَ إِصْبَعَيْنِ مِنْ أَصَابِعِ الرَّحْمَنِ، كَقَلْبٍ وَاحِدٍ، يُصَرِّفُهُ حَيْثُ يَشَاءُ» ثُمَّ قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «اللهُمَّ مُصَرِّفَ الْقُلُوبِ صَرِّفْ قُلُوبَنَا عَلَى طَاعَتِكَ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2654]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi bin Amri bin Aaswi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake akisema:
"Hakika nyoyo za wanadamu zote ziko baina ya vidole viwili miongoni mwa vidole vya Rahmaan (Mwingi wa rehema), kama moyo wa mtu mmoja, anaugeuza kokote atakako" Kisha akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu mwenye kuzigeuza nyoyo, zigeuze nyoyo zetu zielekee katika kukutii".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2654]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa nyoyo za wanadamu zote ziko baina ya vidole viwili katika vidole vya Rahmaan kama moyo mmoja; anaugeuza kokote atakako; akitaka anausimamisha katika haki, na akitaka anaupotoa katika haki, na kuzigeuza kwake nyoyo zote ni kama kuugeuza moyo mmoja, hakuna jambo linaloweza kumshughulisha akaacha jambo jingine, kisha akaomba rehema na amani ziwe juu yake akasema: Ewe Mwenyezi Mungu mwenye kuzigeuza nyoyo, wakati mwingine katika utiifu na wakati mwingine katika maasi, na wakati mwingine katika kukutaja na wakati mwingine katika kughafilika, zigeuze nyoyo zetu zielekee katika utiifu wako.