عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ:
قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ اللَّهَ قَالَ: مَنْ عَادَى لِي وَلِيًّا فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالحَرْبِ، وَمَا تَقَرَّبَ إِلَيَّ عَبْدِي بِشَيْءٍ أَحَبَّ إِلَيَّ مِمَّا افْتَرَضْتُ عَلَيْهِ، وَمَا يَزَالُ عَبْدِي يَتَقَرَّبُ إِلَيَّ بِالنَّوَافِلِ حَتَّى أُحِبَّهُ، فَإِذَا أَحْبَبْتُهُ: كُنْتُ سَمْعَهُ الَّذِي يَسْمَعُ بِهِ، وَبَصَرَهُ الَّذِي يُبْصِرُ بِهِ، وَيَدَهُ الَّتِي يَبْطِشُ بِهَا، وَرِجْلَهُ الَّتِي يَمْشِي بِهَا، وَإِنْ سَأَلَنِي لَأُعْطِيَنَّهُ، وَلَئِنِ اسْتَعَاذَنِي لَأُعِيذَنَّهُ، وَمَا تَرَدَّدْتُ عَنْ شَيْءٍ أَنَا فَاعِلُهُ تَرَدُّدِي عَنْ نَفْسِ المُؤْمِنِ، يَكْرَهُ المَوْتَ وَأَنَا أَكْرَهُ مَسَاءَتَهُ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 6502]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Hakika Mwenyezi Mungu amesema: Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi nitakuwa nimemtangazia vita, na hatojiweka karibu kwangu mja kwa kitu ninachokipenda katika vile nilivyomfaradhishia juu yake, na akawa bado mja wangu anaendelea kujiweka karibu yangu kwa ibada za sunna (zisizokuwa za lazima) mpaka nitafikia mahala nitampenda, nikishampenda: Nitakuwa sikio lake analosikilizia, na jicho lake analotazamia, na mkono wake anaoshikia, na mguu wake anaotembelea, na hata akiniomba hakika nitampa, na hata akinitaka kinga hakika nitamlinda, na sijawahi kusita katika jambo lolote ninalotaka kulifanya kama kusita kwangu katika (kuitoa) nafsi ya muumini, hapendi kufa na mimi sipendi kumuudhi".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 6502]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika hadithil Qudsi yakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: Atakayemuudhi kipenzi miongoni mwa vipenzi vyangu na akamkasirisha na akambughudhi basi nitakuwa nimemtangazia uadui.
Na walii (Kipenzi) ni: Muumini mchamungu, na kwa kadiri imani na uchamungu wa mja unavyokuwa ndivyo nafasi yake ya ukaribu inavyokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Na hajawahi muislamu kujiweka karibu kwa Mola wake kwa jambo alipendalo zaidi kuliko lile alilomfaradhishia na akamuwajibishia juu yake, ikiwemo kufanya mambo yote ya utiifu, na kuacha maharamisho, na kwa kadiri anavyoendelea muislamu kujikurubisha kwa Mola wake kwa yale ya sunna pamoja na faradhi; mpaka atapata mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu akimpenda, atakuwa akimtimizia mambo yake katika viungo hivi vinne:
Atampa umakini katika kusikia kwake, hatosikia ila yale yenye kumridhisha Mwenyezi Mungu.
Na humpa umakinifu katika macho yake, hatotazama ila yale anayoyapenda Mwenyezi Mungu kuyatazama na anayaridhia.
Na anampa umakinifu katika mkono wake, hatofanya kwa mkono wake ila yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu.
Na anampa umakinifu katika mguu wake, hatokwenda ila katika yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu, na wala hatoyaendea ila yale yenye kheri ndani yake.
Pamoja na haya yote, akimuomba Mwenyezi Mungu chochote basi Mwenyezi Mungu humpa alichoomba, anakuwa ni mtu mwenye kujibiwa maombi, na ikiwa atataka hifadhi kwa Mwenyezi Mungu na akaomba ulinzi kwake kwa kutaka hifadhi, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu humkinga dhidi ya yale anayoyahofu.
Kisha akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Na sijawahi kusita katika jambo ninalotaka kulifanya kama kusita kwangu katika kuichukua nafsi ya muumini, kwa kumhurumia; kwa sababu yeye anachukia kifo kwa kuwa ndani yake kuna maumivu, na Mwenyezi Mungu hapendi yanayomuudhi muumini.