عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«اثْنَتَانِ فِي النَّاسِ هُمَا بِهِمْ كُفْرٌ: الطَّعْنُ فِي النَّسَبِ، وَالنِّيَاحَةُ عَلَى الْمَيِّتِ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 67]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Mambo mawili kwa watu hayo kwao ni ukafiri: Kutiana doa katika nasaba (ukoo), na kulia kwa kumuomboleza maiti".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 67]
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mambo mawili kwa watu kuwa ni katika matendo ya makafiri, na ni tabia za enzi za ujinga, nayo ni:
La kwanza: Kutukana nasaba (koo) za watu na kuzishushia heshima na kujikweza juu yao.
La pili: Kunyanyua sauti wakati wa msiba kwa kulalamika juu ya kadari, au kukata nguo kwa sababu ya mfadhaiko mkubwa.