عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَنْ حَلَفَ فَقَالَ فِي حَلِفِهِ: وَاللَّاتِ وَالعُزَّى، فَلْيَقُلْ: لاَ إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَمَنْ قَالَ لِصَاحِبِهِ: تَعَالَ أُقَامِرْكَ، فَلْيَتَصَدَّقْ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 4860]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Atakaye apa akasema katika kiapo chake: Na apa kwa Lata na uzza, basi aseme: Hapana apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na atakayesema kumwambia ndugu yake: Njoo tucheze kamari, basi na atoe sadaka".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 4860]
Anatahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuapa kwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu; kwani muumini haapi ila kwa Mwenyezi Mungu, Na anaeleza kuwa atakayeapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu; Kwa mfano mtu akiapa kwa Lata na Uzza - masanamu mawili yaliyokuwa yakiabudiwa katika zama za kabla ya Uislamu - basi aseme ndani ya nafsi yake: Hapana apasayekuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, ili ajiepushe na ushirikina na ili iwe ni fidia ya kiapo chake hicho.
Kisha akaeleza rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayemwambia rafiki yake: Njoo tucheze kamari - ambayo ni watu wawili au zaidi watakaposhindana kwa sharti kuwa baina yao kuna pesa ambayo mshindi ataichukua, na kila mmoja wao lazima ima apate hasara au faida-; ni sunna atoe sadaka kwa kitu chochote kama kafara ya yale aliyoyahamasisha.