عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعًا: «إِنَّ الله -تَعَالى- يَغَارُ، وغَيرَةُ الله -تَعَالَى-، أَنْ يَأْتِيَ المَرء ما حرَّم الله عليه».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, Hadithi Marfu'u: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anapata wivu, na wivu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni kuyafanya mtu yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu kwake yeye"
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Imekuja hadithi ili ibainishe kuwa Mwenyezi Mungu anapata wivu juu ya Maharamisho yake, anachukia na anakereka kuvunjwa mipaka yake, na katika hayo ni uchafu wa zinaa, hiyo ni njia ya udhalili na mbaya, na kisha Mwenyezi Mungu akawaharamishia waja wake zinaa na njia zake zote, mja atakapozini basi Mwenyezi Mungu anakuwa na wivu (anaghadhibika na kuchukia) zaidi na vikubwa mno kuliko anavyochukia katika mambo mengine katika maharamisho, hivyo hivyo hata kulawiti, nako ni kumwendea mwanaume kwa matamanio, kwani hili ni kubwa na ni kubwa zaidi kuliko zinaa; na kwasababu hiyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akalifanya kuwa ni chafu baya zaidi kuliko zinaa. Na hivyo hivyo pia wizi na kunywa pombe na maharamisho yote Mwenyezi Mungu hupata wivu kutokana nayo, lakini baadhi ya maharamisho unakuwa wivu wake ni mkubwa zaidi kuliko mengine, inategemeana na ovu, na inategemeana na madhara yanayoambatana na hilo.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. kuchukizwa na kufanya maharamisho; kwasababu yana mkasirisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  2. Kuthibitisha wivu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu-kwa namna inayomstahiki- Aliyetakasika na Kutukuka.
  3. Ni mtu kuhisi anaangaliwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu- na kuogopa ghadhabu zake, yanapovamiwa maharamisho yake.
Ziada