عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«لَتَتَّبِعُنَّ سَنَنَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ، شِبْرًا بِشِبْرٍ، وَذِرَاعًا بِذِرَاعٍ، حَتَّى لَوْ دَخَلُوا فِي جُحْرِ ضَبٍّ لَاتَّبَعْتُمُوهُمْ» قُلْنَا: يَا رَسُولَ اللهِ آلْيَهُودَ وَالنَّصَارَى؟ قَالَ: «فَمَنْ؟».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 2669]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khuduriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
“Hakika mtafuata njia za walio kuwa kabla yenu, hatua kwa hatua, na dhiraa kwa dhiraa, hata wakiingia kwenye pango la mburukenge, mtawafuata.” Tukasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, unakusudia Mayahudi na Wakristo? Akasema: “Kwa hiyo ni nani?”
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 2669]
Anaeleza rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, jinsi hali ya baadhi ya watu wa Umma wake watakavyokuwa baada ya zama zake, ambako ni kufuata njia ya Mayahudi na Wakristo katika imani, matendo, desturi na mila zao, kufuata kwa undani sana, inchi kwa inchi, na dhiraa kwa dhiraa, hata wakiingia katika tundu la mburukenge, nao wataingia nyuma yao.