عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعًا: «إِذَا لَبِسْتُم، وَإِذَا تَوَضَّأتُم، فَابْدَأُوا بَأَيَامِنُكُم».
[صحيح] - [رواه أبو داود واللفظ له، والترمذي وابن ماجه وأحمد]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Mtakapo vaa, na mtakapo tawadha, basi anzeni na kuliani kwenu".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na Ahmad]
Imetilia mkazo hadithi ya Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake swala la kuanza na kulia katika mambo mazuri, ikapokelewa kuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Mtakapo vaa" Yaani mkitaka kuvaa. "Na mtakapo tawadha" Yaani mkitaka kufanya. "Anzeni na kuliani kwenu" ni wingi wa kulia nacho ni kinyume cha kushoto, aingize upande wa kulia wa kanzu, kabla ya kushoto na atangulize kulia katika mikono yake na miguu yake katika udhu, kisha tambua kuwa katika viungo vya udhu vipo ambavyo si sunna kuanza na kulia, navyo ni masikio mawili na viganja viwili na mashavu mawili, bali husafishwa vyote kwa wakati mmoja, ikiwa litakuwa gumu hilo kama ilivyo kwa aliyekatwa mkono na mfano wake atatanguliza kulia.