عن أبي هريرة رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم : "لاَ يَقْبَل الله صلاَة أَحَدِكُم إِذا أَحْدَث حَتَّى يَتوضَّأ".
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Amesema: Amesema Mtume Rehema na Amani zimfikie: "Haikubali Mwenyezi Mungu swala ya mmoja wenu atakapotengukwa udhu mpaka atawadhe".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Sheria tukufu imemuelekeza Mwenye kutaka kuswali, asiingie kusali ispokuwa anapokuwa katika hali nzuri na muonekano mzuri, kwasababu ndio kiunganishi kizito kati ya mja na Mola wake, na ndio njia ya kuelekea kuzungumza naye, hivyo ameamrisha kutia udhu na kufanya usafi, na akamueleza kuwa swala inakataliwa na wala haikubaliwi pasina kuwa na twahara.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kutukuzwa kwa jambo la swala, kiasi ambacho Mwenyezi Mungu haikubali ila mpaka iwe pamoja na twahara.
  2. Swala ya mtu aliyetengukwa udhu haikubaliki mpaka ajitwaharishe kutokana na haja mbili, kubwa na ndogo.
  3. Uchafu unatengua udhu na unabatilisha swala, ukiwa ndani yake.
  4. Makusudio ya kutokubalika hapa: ni kutosihi swala na kutolipwa.
  5. Inafaidisha hadithi kuwa swala ziko zinazokubalika na ziko zinazorejeshwa, zitakazokuwa zimeafikiana na sheria basi zitakubalika, na zitakazokuwa kinyume na sheria zitarejeshwa, na hivyo hivyo ibada zote; kwa kauli ya Mtume Rehema na Amani zimfikie: "Atakayefanya jambo lolote lisilokuwa ndani yake na mafundisho yetu basi litarejeshwa".
  6. Swala ya mwenye hadathi (aliyetengukwa udhu) ni haramu mpaka atawadhe; kwasababu Mwenyezi Mungu haikubali, na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa yale asiyoyakubali ni kupingana naye, na ni aina ya kufanya mzaha.
  7. Mtu atakapotawadha kwaajili ya swala, kisha ukamfikia muda wa swala nyingine, naye akiwa bado yuko katika twahara yake haimlazimu kwake kutia udhu mara ya pili.
  8. Swala ya faradhi na ya sunna hata swala ya jeneza haikubaliki atakapoiswali asiyekuwa na udhu hata kama atakuwa kasahau mpaka atawadhe, hivyo hivyo hata mwenye janaba atakaposwali kabla hajaoga, na inamlazimu aliyesahau kuirudia.