عن حذيفة بن اليمان رضي الله عنهما عن رسول الله صلى الله عليه وسلم أنه قال: «وَالَّذِي نَفسِي بِيَدِه، لَتَأْمُرُنَّ بِالمَعرُوف، وَلَتَنهَوُنَّ عَنِ المُنْكَر؛ أَو لَيُوشِكَنَّ الله أَن يَبْعَثَ عَلَيكُم عِقَاباً مِنْه، ثُمَّ تَدعُونَه فَلاَ يُسْتَجَابُ لَكُم».
[حسن] - [رواه الترمذي وأحمد]
المزيــد ...

Kutoka kwa Hudhaifa bin Yamani -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakwamba yeye alisema; "Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mtaamrisha mema, na mtakataza mabaya; au hakika atakuwa karibu zaidi Mwenyezi Mungu kukutumieni adhabu toka kwake, kisha mtamuomba na wala hamtojibiwa".
Ni nzuri - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy

Ufafanuzi

Kauli yake -Rehema na Amani ziwe juu yake-"Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake" Hiki ni kiapo anaapa Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa Mwenyezi Mungu; kwasababu yeye ndiye ambaye nafsi za waja ziko mkononi mwake -Ametakasika na kutukuka-Anaziongoza akitaka, na anazipoteza akitaka, na anazifisha akitaka, na anazibakisha akitaka, hivyo nafsi zote ziko mkononi mwa Mwenyezi Mungu katika uongofu na upotovu, na kuzihuisha na kuzifisha na maamuzi na mipangilio katika kila kitu, kama alivyosema Mtukufu aliyetakasika-: "Na ninaapa kwa nafsi (roho) na aliyeiumba, Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake), Hivyo nafsi ziko mkononi mwa Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake; na kwasababu hii aliapa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-, Na alikuwa mara nyingi akiapa kwa kiapo hiki: (Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake), na wakati mwingine alikuwa akisema: (Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammad iko mkononi mwake); kwasababu nafsi ya Muhammad ndio nafsi safi zaidi kuliko zote, akaapa kwa hilo; kwakuwa ni nafsi safi. Kisha akataja alichokiapia, nacho nikuwa tusimamie kuamrisha mema na kukataza maovu; au vinginevyo atufunike Mwenyezi Mungu kwa adhabu itokayo kwake, mpaka ifikie mahali tunamuomba na wala hatukubalii, Na huu ni uwazi juu umuhimu wa kuamrisha mema kama swala na zaka na kutimiza haki, na umuhimu wa kukataza mabaya kama zinaa na riba na maharamisho mengine, na hii inakuwa kwa vitendo kwa yule ambaye ana mamlaka kama baba katika nyumba yake na mgambo wenye jukumu hilo na polisi, au kwa kauli nzuri na hili ni kwa kila mtu, au kuchukia kwa moyo pamoja na kuondoka mahala palipo na uovu, na hii ni kwa yule asiyeweza kukemea kwa vitendo au kwa kauli.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kireno
Kuonyesha Tarjama