عن أبي بكر الصديق رضي الله عنه قال: يا أيُّها النَّاس، إِنَّكُم لَتَقرَؤُون هذه الآية: (يَا أَيُّها الَّذِين آمَنُوا عَلَيكُم أَنفسَكُم لاَ يَضُرُّكُم مَنْ ضَلَّ إِذَا اهْتَدَيتُم) [المائدة: 105]، وَإِنِّي سمِعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «إِنَّ النَّاس إِذا رَأَوُا الظَّالِمَ فَلَم يَأْخُذُوا عَلَى يَدَيه أَوشَكَ أَنْ يَعُمَّهُمُ اللهُ بِعِقَابٍ مِنْهُ».
[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي وابن ماجه وأحمد]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abubakari Swiddiq, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, ya kwamba yeye alisema: Enyi watu! Hakika nyinyi mnasoma aya hii: "Enyi mlioamini lililo lazima juu yenu ni nafsi zenu hatokudhuruni aliyepotoka ikiwa mtaongoka", na hakika mimi nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akisema:
"Hakika watu wakimuona dhalimu na wasimchukulie hatua, basi wako karibu Mwenyezi Mungu kuwaadhibu wote kwa adhabu yake."
[Sahihi] - - [سنن الترمذي - 2168]
Anasimulia Abubakari Swiddiq, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, kuwa watu wanasoma aya hii:
"Enyi mlioamini lililo lazima juu yenu ni nafsi zenu hatokudhuruni aliyepotoka ikiwa mtaongoka" [Maaida: 105]
Na wanaielewa kuwa mtu anatakiwa ajitume kuirekebisha nafsi yake pekee, na kwamba hatodhurika baada ya hapo kwa upotofu wa wale waliopotea, na kuwa hawajaamrishwa kuamrisha mema na kukataza maovu!
Basi akawajulisha kuwa haikuwa hivyo, na kwamba alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Iwapo watu watamuona dhalimu na wasimzuie na dhulma yake, na hali yakuwa wana uwezo wa kumzuia, basi Mwenyezi Mungu yuko karibu kueneza adhabu kutoka kwake kwa wote, anayefanya uovu na anayenyamaza juu yake.