عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قَالَ:
«لَا يَمْنَعَنَّ رَجُلًا مِنْكُمْ مَخَافَةُ النَّاسِ أَنْ يَتَكَلَّمَ بِالْحَقِّ إِذَا رَآهُ أَوْ عَلِمَهُ».
[صحيح] - [رواه الترمذي وابن ماجه وأحمد] - [مسند أحمد: 11403]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Kusimzuie mmoja wenu kuwaogopa watu akaache kusema haki atakapoiona au kuijua".
[Sahihi] - - [مسند أحمد - 11403]
Alihutubia Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Maswahaba zake, na miongoni mwa mambo aliyowausia ni kuwa Muislamu isimzuie hofu na kuowaogopa watu na nguvu yao akaacha kusema haki au kuiamrisha atakapoiona au kuijua.