عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«قَالَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ: يُؤْذِينِي ابْنُ آدَمَ يَسُبُّ الدَّهْرَ وَأَنَا الدَّهْرُ، بِيَدِي الأَمْرُ أُقَلِّبُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 4826]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ananiudhi mimi mwanadamu, anatukana nyakati na mimi ndiye nyakati, ninaugeuza usiku na mchana".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 4826]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika Hadithil Kudsi: Ananiudhi na ananishusha hadhi mwanadamu anayetukana na kusema vibaya wakati wa kufikwa na matatizo na machukizo; kwa sababu yeye Mtukufu ndiye mpangiliaji peke yake na muendeshaji wa yote yanayotokea; kutukana nyakati ni kumtukana Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na nyakati ni kiumbe na kinaendeshwa, yanatokea matukio ndani yake kwa amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.