عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ عُمَرَ رَضيَ اللهُ عنهُما قَالَ: مَرَرْنَا مَعَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى الْحِجْرِ، فَقَالَ لَنَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«لَا تَدْخُلُوا مَسَاكِنَ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَنْفُسَهُمْ، إِلَّا أَنْ تَكُونُوا بَاكِينَ؛ حَذَرًا أَنْ يُصِيبَكُمْ مِثْلُ مَا أَصَابَهُمْ» ثُمَّ زَجَرَ فَأَسْرَعَ حَتَّى خَلَّفَهَا.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 2980]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abdallah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake, amesema: Tulipita tukiwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika Hijiri (miji ya Thamudi), akasema kutuambia Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Msiingie miji ya wale waliozidhulumu nafsi zao, isipokuwa muwe mnalia; kwa kutahadhari msijekupatwa na mfano wa yale yaliyowapata" Kisha akampigia kelele mnyama wake akaongeza mwendo mpaka akapapita.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 2980]
Alikataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipopita katika miji ya Thamudi, kutoingia katika miji ya walioadhibiwa, wale waliozidhulumu nafsi zao au kuiendea miji hiyo, isipokuwa anayeingia kama atakuwa analia kwa kuchukua mazingatio kwao; kwa kuhofia asijekufikwa na mfano wa yale yaliyowafika miongoni mwa adhabu, kisha akampigia kelele mnyama wake akaongeza mbio mpaka akaivuka.