عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنِينَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْها أَنَّهَا قَالَتْ:
أَوَّلُ مَا بُدِئَ بِهِ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنَ الوَحْيِ الرُّؤْيَا الصَّالِحَةُ فِي النَّوْمِ، فَكَانَ لاَ يَرَى رُؤْيَا إِلَّا جَاءَتْ مِثْلَ فَلَقِ الصُّبْحِ، ثُمَّ حُبِّبَ إِلَيْهِ الخَلاَءُ، وَكَانَ يَخْلُو بِغَارِ حِرَاءٍ فَيَتَحَنَّثُ فِيهِ -وَهُوَ التَّعَبُّدُ- اللَّيَالِيَ ذَوَاتِ العَدَدِ قَبْلَ أَنْ يَنْزِعَ إِلَى أَهْلِهِ، وَيَتَزَوَّدُ لِذَلِكَ، ثُمَّ يَرْجِعُ إِلَى خَدِيجَةَ فَيَتَزَوَّدُ لِمِثْلِهَا، حَتَّى جَاءَهُ الحَقُّ وَهُوَ فِي غَارِ حِرَاءٍ، فَجَاءَهُ المَلَكُ فَقَالَ: اقْرَأْ، قَالَ: «مَا أَنَا بِقَارِئٍ» قَالَ: «فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي حَتَّى بَلَغَ مِنِّي الجَهْدَ ثُمَّ أَرْسَلَنِي، فَقَالَ: اقْرَأْ، قُلْتُ: مَا أَنَا بِقَارِئٍ، فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي الثَّانِيَةَ حَتَّى بَلَغَ مِنِّي الجَهْدَ ثُمَّ أَرْسَلَنِي، فَقَالَ: اقْرَأْ، فَقُلْتُ: مَا أَنَا بِقَارِئٍ، فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي الثَّالِثَةَ ثُمَّ أَرْسَلَنِي، فَقَالَ: {اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ خَلَقَ الإِنْسَانَ مِنْ عَلَقٍ اقْرَأْ وَرَبُّكَ الأَكْرَمُ}»، [العلق:1-3] فَرَجَعَ بِهَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَرْجُفُ فُؤَادُهُ، فَدَخَلَ عَلَى خَدِيجَةَ بِنْتِ خُوَيْلِدٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا، فَقَالَ: «زَمِّلُونِي، زَمِّلُونِي» فَزَمَّلُوهُ حَتَّى ذَهَبَ عَنْهُ الرَّوْعُ، فَقَالَ لِخَدِيجَةَ وَأَخْبَرَهَا الخَبَرَ: «لَقَدْ خَشِيتُ عَلَى نَفْسِي» فَقَالَتْ خَدِيجَةُ: كَلَّا وَاللَّهِ مَا يُخْزِيكَ اللَّهُ أَبَدًا، إِنَّكَ لَتَصِلُ الرَّحِمَ، وَتَحْمِلُ الكَلَّ، وَتَكْسِبُ المَعْدُومَ، وَتَقْرِي الضَّيْفَ، وَتُعِينُ عَلَى نَوَائِبِ الحَقِّ، فَانْطَلَقَتْ بِهِ خَدِيجَةُ حَتَّى أَتَتْ بِهِ وَرَقَةَ بْنَ نَوْفَلِ بْنِ أَسَدِ بْنِ عَبْدِ العُزَّى، ابْنَ عَمِّ خَدِيجَةَ، وَكَانَ امْرَأً تَنَصَّرَ فِي الجَاهِلِيَّةِ، وَكَانَ يَكْتُبُ الكِتَابَ العِبْرَانِيَّ، فَيَكْتُبُ مِنَ الإِنْجِيلِ بِالعِبْرَانِيَّةِ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَكْتُبَ، وَكَانَ شَيْخًا كَبِيرًا قَدْ عَمِيَ، فَقَالَتْ لَهُ خَدِيجَةُ: يَا ابْنَ عَمِّ، اسْمَعْ مِنَ ابْنِ أَخِيكَ، فَقَالَ لَهُ وَرَقَةُ: يَا ابْنَ أَخِي، مَاذَا تَرَى؟ فَأَخْبَرَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خَبَرَ مَا رَأَى، فَقَالَ لَهُ وَرَقَةُ: هَذَا النَّامُوسُ الَّذِي نَزَّلَ اللَّهُ عَلَى مُوسَى، يَا لَيْتَنِي فِيهَا جَذَعًا، لَيْتَنِي أَكُونُ حَيًّا إِذْ يُخْرِجُكَ قَوْمُكَ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَوَ مُخْرِجِيَّ هُمْ؟»، قَالَ: نَعَمْ، لَمْ يَأْتِ رَجُلٌ قَطُّ بِمِثْلِ مَا جِئْتَ بِهِ إِلَّا عُودِيَ، وَإِنْ يُدْرِكْنِي يَوْمُكَ أَنْصُرْكَ نَصْرًا مُؤَزَّرًا. ثُمَّ لَمْ يَنْشَبْ وَرَقَةُ أَنْ تُوُفِّيَ، وَفَتَرَ الوَحْيُ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 3]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:
Jambo la kwanza alilioanza kupewa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake katika wahyi, ni njozi nzuri (za kweli) usingizini. Akawa haoti njozi isipokuwa itatokea, mfano wa mapambazuko ya asubuhi, kisha akapendezeshwa kujitenga peke yake katika pango la Hira, akawa akitawa huko - ambako ni kuabudu - kwa siku kadhaa, kabla ya kurejea katika familia yake, na alikuwa akichukua chakula cha kutosha kwa ajili ya hilo, kisha alikuwa akirudi kwa Khadija na kumpatia chakula mfano wa hicho, mpaka ukweli ukamjia akiwa ndani ya pango la Hira, Malaika akamjia, akasema: "Soma!" akasema: “Mimi si msomaji.” Akanichukua na akanifunika mpaka nikachoka, kisha akaniacha, akasema: "Soma!" Nikasema: “Mimi sio msomaji". Basi akanichukua na akanifunika mara ya pili mpaka nikapatwa na uchovu, kisha akaniacha, kisha akasema: "Soma!" nikasema: "Mimi si msomaji", basi akanichukua na akanifunika kwa mara ya tatu, kisha akaniacha, na akasema: "Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba Amemuumba mwanadamu kwa pande la damu Soma na Mola wako Mlezi ni Mkarimu" [Al-Alaq: 1-3] Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akarudi huku moyo wake ukitetemeka, akaingia kwa Khadija binti Khuwailidi, Allah amuwiye radhi, na akasema: “Nisaidieni, kuwa pamoja nami, Nisaidieni, kuwa pamoja nami” Basi wakamkumbatia mpaka hofu ikamtoka, basi akamwambia Khadija na kumueleza habari hiyo: “Nilihofia sana nafsi yangu" Khadija akasema: Hapana, Wallahi kamwe Mwenyezi Mungu hatokufedhehesha, hakika wewe utaunga udugu, utamsaidia mnyonge, na utaleta kilichokosekana, na utamkirimu mgeni, na utasaidia wakati wa matatizo ya haki, basi Khadija akaondoka naye mpaka wakafika kwa Waraqa bin Nawfal bin Asad bin Abdil-Uzza, binamu yake Khadija, na alikuwa ni mtu aliyeingia katika Ukristo wakati wa kabla ya Uislamu, na alikuwa akiandika vitabu vya Kiebrania, hivyo aliandika kutoka katika Injili kwa Kiebrania, kiasi alichotaka Mwenyezi Mungu akiandike, alikuwa mzee ambaye amekwisha pofuka, basi Khadija akamwambia: Ewe binamu, sikia kutoka kwa mtoto wa ndugu yako. Waraqa akamuuliza: Ewe mpwa wangu, unaona nini? Basi Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akamueleza aliyoyaona. Waraqa akamwambia: Hii ndiyo sheria aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu kwa Musa. Hakika ninatamani ningekuwa hai wakati watu wako, pindi watakapokufukuza watu wako. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: “Hivi, kwani watanifukuza!?" Akasema: "Ndiyo" Kamwe hakuwahi kuja mtu na kitu kama ulichokuja nacho, isipokuwa alitendewa uadui, na ikiwa siku yako hiyo itanifikia nikiwa hai, basi nitakutetea utetezi wa nguvu. Kisha Waraqa hakuchukua muda mrefu akawa amefariki, na wahyi ukasimama kuteremka kwa muda.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 3]
Ameeleza mama wa Waumini, Aisha, Allah amuwiye radhi, kwamba jambo la kwanza aliloanziwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni njozi za kweli usingizini, akawa haoti kitu katika njozi zake isipokuwa kilitokea wazi mfano wa nuru ya asubuhi, kisha akapendezeshwa kujitenga, na alikuwa akijitenga ndani ya pango la Hiraa akifanya ibada kwa siku kadhaa, kabla ya kurudi katika familia yake, na alikuwa akichukua chakula cha kumtosheleza, kisha anarejea kwa mama wa waumini Khadija radhi za Allah ziwe juu yake, anachukua tena chakula cha kutosha idadi ya siku kama hizo, mpaka ikamjia amri ya kweli, naye akiwa katika pango la Hira. Kisha akamjia Malaika Jibril amani iwe juu yake, akamwambia: Soma, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Mimi si mzuri katika kusoma, anasema: Akanishika akanibana mpaka nikachoka na kuishiwa nguvu, kisha akaniachia na kusema: Soma. Nikasema: Mimi si mzuri katika kusoma, basi akanichukua na kunibana kwa mara ya pili mpaka nikachoka na kuishiwa nguvu, kisha akaniacha, akasema: Soma. Nikasema: Sijui kusoma, basi akanichukua na akanifunika mara ya tatu, kisha akaniacha na akasema: "Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliyeumba. Kamuumba mwanadamu kutokana na pande la nyama. Soma na Mola wako Mlezi ni Mkarimu" [Al-Qalaq: 1-3]. Akarejea Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa na aya kadhaa, lakini kifua chake kilikuwa kikitetemeka kwa kuhofia kifo, akaingia kwa mkewe mama wa waumini Khadija binti Khuwailidi radhi za Allah ziwe juu yake akasema: Nifunikeni na nguo, nifunikeni na nguo, wakamfunikwa kwa nguo mpaka hofu ikamuondokea, akasema kumwambia Khadija na akampa habari ya kilichotokea, na akasema: Nilihofia kifo juu ya nafsi, Khadija akasema: Si hivyo, Wallahi hawezi kukufedhehesha Mwenyezi Mungu kamwe! Hakika wewe utaunga udugu, na utamsaidia mnyonge ambaye jambo lake halina muelekeo, na utamnyanyua fakiri asiye na kitu; kiasi ambacho utawapa watu yale wasiyoyapata kwa asiyekuwa wewe, na utamkirimu mgeni, na utasaidia kutatua matatizo ya haki. Khadija akamchukua mpaka akamfikisha kwa Waraqa bin Naufali bin Asadi bin Abdil -Uzza, ambaye ni mtoto wa ami yake, na alikuwa ni mtu aliyeachana na mila za kale na akawa mkristo, na alikuwa akiandika kutoka katika Injili kwa lugha ya Kiebrania kiasi alichokitaka Mwenyezi Mungu akiandike, na alikuwa ni mzee mtu mzima aliyepofuka macho yake, Khadija akasema kumwambia: Ewe mtoto wa ammi, hebu msikilize mtoto wa ndugu yako, Waraqa akasema kumwambia: Ewe mtoto wa ndugu yangu, umeona nini? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamueleza habari ya kile alichokiona, Waraqa akasema kumwambia: Huyo ni Malaika Jibrili aliyemteremsha Mwenyezi Mungu kwa Musa amani iwe juu yake, natamani lau ningekuwa wakati huo ni kijana mwenye nguvu, laiti kama nitakuwa hai, wakati wakikufukuza watu wako, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hivi, kwani wao watanifukuza?!. Akasema: Ndiyo, kamwe hajawahi kuja mtu na mfano wa hiki ulichokujanacho isipokuwa aliudhiwa na kutendewa uadui, na ikiwa siku yako hiyo itanikuta nikiwa hai basi nitakutetea utetezi wa nguvu. Kisha hakukaa muda mrefu Waraqa akawa amefariki, na wahyi ukachelewa kuteremka tena kwa muda kidogo.