+ -

عَنْ أبي سَلَمَةَ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ أَنَّ جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ الأَنْصَارِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: وَهُوَ يُحَدِّثُ عَنْ فَتْرَةِ الوَحْيِ، فَقَالَ فِي حَدِيثِهِ:
«بَيْنَا أَنَا أَمْشِي إِذْ سَمِعْتُ صَوْتًا مِنَ السَّمَاءِ، فَرَفَعْتُ بَصَرِي، فَإِذَا المَلَكُ الَّذِي جَاءَنِي بِحِرَاءٍ جَالِسٌ عَلَى كُرْسِيٍّ بَيْنَ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ، فَرُعِبْتُ مِنْهُ، فَرَجَعْتُ فَقُلْتُ: زَمِّلُونِي، فَأَنْزَلَ اللَّهُ تَعَالَى: {يَا أَيُّهَا المُدَّثِّرُ1 قُمْ فَأَنْذِرْ} [المدثر: 2] إِلَى قَوْلِهِ {وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ} [المدثر: 5]. فَحَمِيَ الوَحْيُ وَتَتَابَعَ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 4]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Salama bin Abdilrahman yakwamba Jabiri bin Abdillah Al-Answari radhi za Allah ziwe juu yao, alisema wakati akizungumzia kipindi cha Wahyi, akasema katika hadithi yake:
"Wakati nikiwa natembea ghafla nilisikia sauti kutoka mbinguni, nikanyanyua macho yangu, ghafla yule Malaika aliyenijia nikiwa pango la Hiraa nikamuona amekaa juu ya kiti baina ya mbingu na Ardhi, nikaingiwa hofu kwa ajili yake, nikarudi nikasema: Nifunikeni, Mwenyezi Mungu Mtukufu akateremsha: "Ewe uliyejigubika 1 Simama na uonye" [Mudathiri: 2] Mpaka katika kauli yake: "Na yaliyo machafu yahame" [Mudathiri: 5]. Wahyi ukachemka na ukafululiza"

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 4]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati akielezea kukatika kwa Wahyi na kuzuiwa kushuka kwake mwanzo wa kutumwa kwake: Wakati nikiwa natembea katika mitaa ya Makka ghafla nilisikia sauti kutoka mbinguni, nikanyanyua macho yangu, mara ghafla Malaika Jibril aliyenijia kule pango la Hiraa nikamuona amekaa juu ya kiti baina ya mbingu na Ardhi, nikapata hofu na fadhaa kwa sababu yake, nikarudi kwa familia yangu nikasema: Nifunikeni kwa nguo. Akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Ewe uliyejifunika nguo" uliyejigubika kwa nguo zako, "simama" kwa ajili ya kufikisha ujumbe "Uonye" na umtahadharishe asiyeamini utume wako. "na Mola wako Mlezi" Mungu wako muabudiwa "Umtukuze" na umhimidi na umtukuze. "Na nguo zako" na mavazi yako "yasafishe" yaondoshe najisi, "na machafu" kama kuabudu masanamu na mizimu "ihame" iache, Wahyi ukawa na nguvu baada ya hapo na ukakithiri.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kukatika kwa Wahyi kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa muda kadhaa baada ya kuteremka kwa kauli yake Mtukufu: "Soma".
  2. Inafaa mtu kuzungumzia matukio yaliyomtokea baada kuisha kwake, kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu:
  3. Ya kwanza iliyoteremka ni kauli yake Mtukufu: "Ewe uliyejigubika" baada ya kuteremka: "Soma kwa jina la Mola Mlezi aliyeumba".
  4. Fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake kiasi kwamba alimmiminia wahyi wake pasina kukatika mpaka alipofariki.
  5. Uwajibu wa kusimamia kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuwaonya wapingaji na kuwapa habari njema watiifu.
  6. Uwajibu wa kusafisha nguo kwa ajili ya swala, na wametumia kama ushahidi kauli yake Mtukufu: "Na nguo zako zisafishe".
  7. Uwajibu wa kuamini Malaika na kwa yale aliyowawezesha Mwenyezi Mungu juu yake miongoni mwa matendo na mengineyo.
Tafsiri: Lugha ya Kiindonesia Kibangali Kivetenamu Kikurdi Kireno Thai Kiassam الهولندية الدرية المجرية الجورجية المقدونية
Kuonyesha Tarjama