عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«قَارِبُوا وَسَدِّدُوا، وَاعْلَمُوا أَنَّهُ لَنْ يَنْجُوَ أَحَدٌ مِنْكُمْ بِعَمَلِهِ» قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ وَلَا أَنْتَ؟ قَالَ: «وَلَا أَنَا، إِلَّا أَنْ يَتَغَمَّدَنِيَ اللهُ بِرَحْمَةٍ مِنْهُ وَفَضْلٍ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 2816]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Fanyeni matendo na muwe na msimamo, na tambueni kuwa hatosalimika mmoja wenu kwa sababu ya matendo yake, wakasema: Hata wewe ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?! Akasema: Hata mimi isipokuwa atakaponifunika mimi Mwenyezi Mungu kwa huruma zake na fadhila zake".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 2816]
Anahimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba kufanya amali njema, na wamche Mwenyezi Mungu kadiri wawezavyo, pasina kuchupa mipaka wala uzembe, na wakusudie katika amali zao kupatia kwa kuwa na ikhlasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kufuata mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake ili amali zao zikubaliwe, ili iwe ni sababu ya kuteremka kwa rehema juu yao.
Kisha akawaeleza kuwa amali hazitomuokoa yeyote miongoni mwao kamwe; bali ni lazima kuwe na rehema ya Mwenyezi Mungu.
Wakasema: Hata wewe ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hazitokuokoa amali zako pamoja na ukubwa wa kiwango chake?
Akasema: Hata mimi, ila kama atanisitiri Mwenyezi Mungu kwa fadhila na rehema zake.