عن عمار بن ياسر رضي الله عنهما قال: «بَعَثَنِي النبي صلى الله عليه وسلم في حَاجَة، فَأَجْنَبْتُ، فَلَم أَجِد المَاءِ، فَتَمَرَّغْتُ فِي الصَّعِيدِ، كَمَا تَمَرَّغ الدَّابَّةُ، ثم أَتَيتُ النبي صلى الله عليه وسلم فَذَكَرتُ ذلك له، فقال: إِنَّمَا يَكْفِيك أن تَقُولَ بِيَدَيكَ هَكَذَا: ثُمَّ ضَرَب بِيَدَيهِ الأَرْضَ ضَرْبَةً وَاحِدَةً، ثُمَّ مَسَحَ الشِّمَالَ عَلَى اليَمِينِ، وظَاهِرَ كَفَّيهِ وَوَجهَهُ».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Ammari bin Yasir -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: "Aliniagiza mimi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika haja fulani, nikaeleza hilo kwake, kuwa nilipata janaba, nikawa sikupata maji, nikajigaragaza katika udongo kama anavyojigaragaza mnyama, kisha nikamuendea Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Nikamsimulia hilo, Akasema: Hakika inakutosheleza kusema kwa mikono yako hivi: kisha akapiga kwa mikono yake miwili chini ya ardhi mpigo mmoja, kisha ukapaka mkono wa kushoto juu ya mkono wa kulia, na juu ya viganja vyake na uso wake".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Alimtuma Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Ammar bin Yasir -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- katika safari kwa baadhi ya haja zake, akapatwa na janaba, na hakupata maji ili aoge, na alikuwa hajui hukumu ya kutayammamu kwa mwenye janaba, bali alikuwa anajua hukumu yake kwa mwenye hadathi (uchafu) mdogo; akajitahidi na akadhania kuwa yeye kama alivyofuta kwa udongo baadhi ya viungo vya udhu kutokana na hadathi ndogo, basi ni lazima itakuwa tayamamu ya janaba ni kuueneza udongo mwili mzima; kwa kuchukulia kipimo cha maji; akajigeuza katika udongo mpaka akaueneza mwili mzima na akaswali, alipofika kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na alikuwa katika nafsi yake ana wasiwasi juu ya kile alichokifanya; kwasababu hilo kalifanya kwa jitihada zake, na akalieleza hilo kwake; ili aone je yuko katika usahihi au la? Akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- inakutosheleza badala ya kuueneza mwili mzima kwa udongo, kupiga kwa mikono yako katika ardhi, pigo mmoja, kisha ukafuta kushoto kwako juu ya kulia kwako, na juu ya kiganja chako na uso wako, mfano wa tayammamu ya udhu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Pashto Kiassam السويدية الأمهرية
Kuonyesha Tarjama
Ziada