+ -

عَن أَبِي أُمَامَةَ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتَ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَخْطُبُ فِي حَجَّةِ الوَدَاعِ فَقَالَ:
«اتَّقُوا اللَّهَ رَبَّكُمْ، وَصَلُّوا خَمْسَكُمْ، وَصُومُوا شَهْرَكُمْ، وَأَدُّوا زَكَاةَ أَمْوَالِكُمْ، وَأَطِيعُوا ذَا أَمْرِكُمْ تَدْخُلُوا جَنَّةَ رَبِّكُمْ».

[صحيح] - [رواه الترمذي وأحمد] - [سنن الترمذي: 616]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Umama radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akihutubu katika Hija ya kuaga akasema:
"Mcheni na Allah Mola wenu Mlezi, na salini swala zenu tano, na fungeni mwezi wenu, na tekelezeni zaka zenu, na mtiini mwenye mamlaka kwenu, (Mkiyafanya haya) mtaingia pepo ya Mola wenu".

[Sahihi] - - [سنن الترمذي - 616]

Ufafanuzi

Alihutubia Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ya Arafa, katika Hija ya kuaga, mwaka wa kumi hijiria (tangu kuhama kutoka Makka) na Hija hiyo iliitwa hivyo kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliwaaga watu ndani yake, Na akawaamrisha watu wote wamuogope Mola wao Mlezi kwa kutekeleza amri zake na kuepuka makatazo yake. Na wasali swala tano alizozifaradhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu usiku na mchana. Na wafunge mwezi wa ramadhani. Na wawape zaka ya mali wastahiki wake na wasizifanyie ubahili. Na wawatii aliowafanya Mwenyezi Mungu kuwa viongozi juu yao, pasipokuwa na kumuasi Mwenyezi Mungu, atakayefanya mambo haya yaliyotajwa basi malipo yake ni kuingia peponi.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية التشيكية Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف الأوكرانية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Matendo haya ni katika sababu za kuingia peponi.