عَنْ أُمِّ قَيْسٍ بِنْتِ مِحْصَنٍ رَضيَ اللهُ عنها:
أَنَّهَا أَتَتْ بِابْنٍ لَهَا صَغِيرٍ لَمْ يَأْكُلِ الطَّعَامَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَأَجْلَسَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي حَجْرِهِ، فَبَالَ عَلَى ثَوْبِهِ، فَدَعَا بِمَاءٍ، فَنَضَحَهُ وَلَمْ يَغْسِلْهُ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 223]
المزيــد ...
Kutoka kwa Ummu Qais bint Mihswan -radhi za Allah ziwe juu yake-:
Yakwamba yeye alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa na mtoto wake mdogo hajaanza kula, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamkalisha katika mapaja yake, akakojoa katika nguo yake, akaomba maji, akanyunyizia na wala hakuosha.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 223]
Alikuja mama Kaisi binti Mihswan radhi za Allah ziwe juu yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa na mtoto wake hajaanza kula chakula kutokana na udogo wa umri wake, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamkalisha katika mapaja yake, mtoto akakojoa katika nguo yake rehema na amani ziwe juu yake, akaomba maji, na akanyunyiza katika nguo yake na wala hakuiosha.