عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنه:
أَنَّهُ لَقِيَهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي طَرِيقٍ مِنْ طُرُقِ الْمَدِينَةِ وَهُوَ جُنُبٌ، فَانْسَلَّ فَذَهَبَ فَاغْتَسَلَ، فَتَفَقَّدَهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَلَمَّا جَاءَهُ قَالَ: «أَيْنَ كُنْتَ يَا أَبَا هُرَيْرَةَ؟» قَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، لَقِيتَنِي وَأَنَا جُنُبٌ فَكَرِهْتُ أَنْ أُجَالِسَكَ حَتَّى أَغْتَسِلَ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «سُبْحَانَ اللهِ، إِنَّ الْمُؤْمِنَ لَا يَنْجُسُ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 371]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-:
Ya kwamba alikutana na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika barabara miongoni mwa barabara za mji wa Madina huku akiwa na janaba, akamkwepa na akaenda kuoga, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamtafuta hakumpata, alipomjia akasema: "Ulikuwa wapi ewe Abuu Huraira?" Akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ulikutana nami, nami nikiwa na janaba, sikufurahishwa kukaa na wewe mpaka nioge, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Sub-haana llaah, ametakasika Mwenyezi Mungu, hakika muumini hanajisiki".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 371]
Alikutana Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Abuu Huraira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake katika baadhi ya njia za Madina, na Abuu Huraira alikuwa na janaba, na kwa sababu ya kumuheshimu kwake Mtume rehema na amani ziwe juu yake alichukia kukaa naye na kuzungumza naye hali yakuwa yuko katika hali ile, kwa kudhani kwake kuwa yeye ni najisi, akaenda kwa uficho na akaoga, kisha akarejea na akakaa, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuuliza kuwa alikwenda wapi? Akamueleza kuhusu hali yake, na kwamba yeye alichukia kukaa naye hali yakuwa yeye ni najisi kwa sababu ya janaba, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akastaajabu, na akasema: Hakika muumini ni msafi na wala hanajisiki kwa hali yoyote; akiwa hai na hata wakiwa maiti.