عن ميمونة بنت الحارث رضي الله عنها قالت: "وَضَعتُ لِرسولِ الله صلى الله عليه وسلم وَضُوءَ الجَنَابَة، فَأَكفَأ بِيَمِينِهِ على يساره مرتين -أو ثلاثا- ثم غَسَل فَرجَه، ثُمَّ ضَرَب يَدَهُ بالأرضِ أو الحائِطِ مرتين -أو ثلاثا- ثم تَمَضْمَضَ واسْتَنْشَقَ، وَغَسَلَ وَجهَه وذِرَاعَيه، ثُمَّ أَفَاضَ على رَأسِه الماء، ثم غَسَل جَسَدَه، ثُمَّ تَنَحَّى، فَغَسَل رِجلَيه، فَأَتَيتُه بِخِرقَة فلم يُرِدْهَا، فَجَعَل يَنفُضُ الماء بِيَده".
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Maimuna binti Harithi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: "Kiliwekwa kwaajili ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- chombo cha kuogea janaba, akamimina kwa mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto mara mbili -au tatu- kisha akaosha tupu yake, kisha akapiga kwa mkono wake ardhi au ukuta mara mbili -au tatu- kisha akasukutua na akapandisha maji puani, na akaosha uso wake na muundi wa mkono wake, kisha akamwaga maji juu ya kichwa chake, kisha akaosha mwili wake, kisha akakaa pembeni, akaosha miguu yake, nikamletea kitambaa hakukihitajia, akawa akifuta maji kwa mkono wake".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Katika hadithi anabainisha mama wa waumini Maimuna -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- binti Harithi namna miongoni mwa namna za uogaji wa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- wa janaba, kiasi ambacho yaliwekwa mahala palipoandaliwa kwaajili ya kuoga maji ili ayatumie kuoga, akamimina kwa mkono wake wa kulia juu ya mkono wa kushoto akaiosha mara mbili au tatu, kisha akaosha tupu yake kwaajili ya kuisafisha na yale yaliyoipata katika athari ya janaba, kisha akapiga ardhi au ukuta na akaisugua mara mbili au tatu, kisha akasukutua na akapandisha maji puani na akaosha uso wake na miundi ya mikono yake, kisha akamwaga maji juu ya kichwa chake, kisha akaosha sehemu za mwili wake zilizobakia, kisha akasogea toka mahala alipo akaosha miguu yake sehemu nyingine, kiasi ambacho hakuiosha mwanzo, kisha akamletea kitambaa ili ajifute kwacho, akawa hakukichukua na akawa anafuta maji mwilini mwake kwa mkono wake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno الدرية
Kuonyesha Tarjama