عن حمران مولى عثمان أنَّه رأى عثمان دعا بوَضُوء، فأفرَغ على يَدَيه مِن إنائه، فغَسَلهُما ثلاثَ مرَّات، ثمَّ أدخل يَمينَه في الوَضُوء، ثمَّ تَمضمَض واستَنشَق واستَنثَر، ثُمَّ غَسل وَجهه ثَلاثًا، ويديه إلى المرفقين ثلاثا، ثم مسح برأسه، ثمَّ غَسل كِلتا رجليه ثلاثًا، ثمَّ قال: رأيتُ النَّبِي صلى الله عليه وسلم يتوضَّأ نحو وُضوئي هذا، وقال: (من توضَّأ نحو وُضوئي هذا، ثمَّ صلَّى ركعتين، لا يحدِّث فِيهما نفسه غُفِر له ما تقدَّم من ذنبه).
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...
Kutoka kwa Humran maula othman, yakwamba yeye alimuona othman akiomba chombo cha udhu, akamimina mikononi mwake kutoka katika chombo chake, akaiosha mara tatu, kisha akaingiza mkono wake wa kulia katika chombo cha udhu, kisha akasukutua na akapandisha maji puani na akapenga, kisha kaosha uso wake mara tatu, na mikono yake mpaka katika viwiko viwili mara tatu, kisha akakifuta kichwa chake, kisha akaosha miguu yake yote miwili mara tatu, kisha akasema: Nilimuona Mtume rehema na Amani zimfikie akitawadha mfano wa udhu wangu huu, na akasema: "Yeyote atakayetawadha mfano wa udhu wangu huu, kisha akasali rakaa mbili, na asiizungumzishe ndani ya nafsi yake atasamehewa yaliyotangulia katika madhambi yake".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Imekusanya hadithi hii tukufu juu ya sifa kamili za udhu wa Mtume rehema na Amani zimfikie- Kwasababu othman kwa mafundisho yake mazuri na uzuri wa uelewa wake kawafundisha sifa ya udhu wa Mtume rehema na Amani zimfikie kwa njia ya kitaalamu, ili iweze kufahamika vizuri zaidi, kwani aliomba chombo chenye maji, na ili asiyachafue maji hakuanza kwa kutumbukiza vidole vyake ndani yake, bali alimimina katika mikono yake mara tatu mpaka ikawa misafi, baada ya hapo aliingiza mkono wake wa kulia katika chombo na akachukulia maji akasukutua na akapandisha puani na akapenga, kisha akaosha uso wake mara tatu, kisha akaosha mikono yake pamoja na viwiko vyake mara tatu, kisha akafuta kichwa chake chote mara moja, kisha akaosha miguu yake na fundo mbili mara tatu. Alipomaliza radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake katika zoezi hili na udhu ulio kamili, aliwaeleza kuwa yeye alimuona Mtume rehema na Amani zimfikie alitawadha mfano wa udhu huu, na akawaeleza Mtume rehema na Amani zimfikie kwamba yeyote atakaye tawadha mfano wa udhu wake, na akaswali rakaa mbili, kwa unyenyekevu na kuhudhurisha moyo wake mbele ya Mola wake aliyetakasika na kutukuka ndani ya hizo rakaa mbili, basi bila shaka kwa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu atamlipa kwa udhu huu uliokamilika, na kwa hii swala yenye utakasifu, kwa kumsamehe yaliyotangulia katika madhambi yake.