عن عائشة رضي الله عنها قالت: (كان النبي صلى الله عليه وسلم إذا اغْتَسَلَ من الجَنَابَة غَسَل يديه، ثُمَّ تَوَضَّأ وُضُوءَه للصَّلاة، ثمَّ اغْتَسَل، ثُمَّ يُخَلِّلُ بِيَدَيه شعره، حتى إِذَا ظَنَّ أنَّه قد أَرْوَى بَشَرَتَهُ، أَفَاض عليه الماء ثَلاثَ مرَّات، ثمَّ غَسَل سائر جسده. وكانت تقول: كُنت أغتسِل أنا ورسول الله صلى الله عليه وسلم من إِنَاء واحِد، نَغْتَرِف مِنه جَمِيعًا).
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: (Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapooga janaba, anaosha mikono yake kisha anatawadha udhu wake wa swala kisha anaoga, kisha anaachanisha kwa mkono wake nywele zake, mpaka anapohisi kuwa tayari ngozi yake imeenea maji, anajimwagia maji mara tatu, kisha anaosha mwili wake wote. Na alikuwa akisema (Aisha): Nilikuwa nikioga mimi na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika chombo kimoja, tukichota humo sote).
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Anaeleza Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- sifa ya kuoga kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa yeye alipotaka kuoga janaba alianza kwa kuosha mikono miwili, ili iwe misafi pale atakapotaka kuchukua maji kwaajili ya kujitwaharisha, na anatawadha kama anavyotawadha kwaajili ya swala, na kwakuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa na nywele nyingi, basi alikuwa akiziachanisha kwa mkono wake kukiwa na maji mpaka maji yafikie katika maotea ya nywele, na yakalowanisha ngozi, anamwaga maji kichwani kwake mara tatu kisha anaosha mwili wake wote uliobakia. Pamoja na josho hili lililokamilika, basi yeye kilikuwa kikimtosheleza yeye pamoja na Aisha chombo kimoja, wakichota wote kutoka katika chombo hicho.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kichina Kifursi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama