عن عَبْدِ اللهِ بْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ:
«مَنْ جَاءَ مِنْكُمُ الْجُمُعَةَ فَلْيَغْتَسِلْ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 894]
المزيــد ...
kutoka kwa Abdullahi bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema:
"Atakayekuja miongoni mwenu kwa ajili ya Ijumaa basi na aoge".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 894]
Anasisitiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa atakayetaka kuja kwa ajili ya swala ya Ijumaa basi inapendeza kwake kuoga, mfano wa kuoga kwake josho la janaba.