عَنِ الحُسَينِ بنِ عَلِيٍّ بنِ أَبِي طَالِبٍ رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«الْبَخِيلُ مَنْ ذُكِرْتُ عِنْدَهُ فَلَمْ يُصَلِّ عَلَيَّ».
[صحيح] - [رواه الترمذي والنسائي في الكبرى وأحمد] - [السنن الكبرى للنسائي: 8046]
المزيــد ...
Kutoka kwa Hussein bin Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yao amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Bahili ni yule ambaye nitatajwa mbele yake, akawa hakuniswalia"
[Sahihi] - - [السنن الكبرى للنسائي - 8046]
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuacha kumtakia rehema wakati wa kusikia jina lake au wasifu wake, na akasema: Bahili kamili ni yule nitakayetajwa mbele yake na akawa hakunitakia rehema; na hili ni kwa sababu ya mambo yafuatayo:
La kwanza: Nikuwa ni ubahili kwa kitu ambacho mtu hapati hasara sawa iwe ndogo au kubwa, wala hatoi mali, na wala hatumii nguvu wala juhudi.
La pili: Ni kuifanyia ubahili nafsi yake kwa sababu anainyima malipo ya kumtakia rehema Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake: kwa sababu anapojizuia kumtakia rehema atakuwa kafanya ubahili na kakataa kutimiza haki ya wajibu kwake kuitekeleza, kwa kutekeleza amri na akapata malipo.
La tatu: Kumtakia rehema ndani yake kuna kutimiza haki za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, yeye ndiye aliyetufundisha, na yeye ndiye aliyetuelekeza, na yeye ndiye aliyetuita kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akaja na wahyi huu, na sheria hii, yeye ndiye sababu ya kuongoka kwetu baada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, atakayeacha kumtakia rehema basi atakuwa kamfanyia ubahili Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake kwa kutompa haki ndogo kabisa miongoni mwa haki zake