+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَنِ اغْتَسَلَ يَوْمَ الجُمُعَةِ غُسْلَ الجَنَابَةِ ثُمَّ رَاحَ، فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ بَدَنَةً، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الثَّانِيَةِ، فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ بَقَرَةً، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الثَّالِثَةِ، فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ كَبْشًا أَقْرَنَ، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الرَّابِعَةِ، فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ دَجَاجَةً، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الخَامِسَةِ، فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ بَيْضَةً، فَإِذَا خَرَجَ الإِمَامُ حَضَرَتِ المَلاَئِكَةُ يَسْتَمِعُونَ الذِّكْرَ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 881]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Atakaye koga siku ya Ijumaa josho la janaba, kisha akatoka katika saa ya kwanza ni kana kwamba katoa sadaka ya ngamia, na atakayetoka katika saa ya pili ni kana kwamba katoa sadaka ya ng'ombe, na atakayetoka katika saa ya tatu ni kana kwamba katoa sadaka ya kondoo, na atakayetoka katika saa ya nne ni kana kwamba katoa sadaka ya kuku, na atakaye kwenda katika saa ya tano ni kama katoa yai, akitoka imamu Malaika wanahudhuria kusikiliza ukumbusho".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 881]

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu fadhila za kuwahi kwenda kuswali swala ya Ijumaa mapema. Na kuwasili mapema kunaanza tangu kuchomoza jua hadi kuwasili kwa Imam; Nazo ni saa tano, na zinagawanywa katika sehemu tano kulingana na muda kati ya kuchomoza kwa jua mpaka kuingia kwa imamu na kupanda kwake juu ya mimbari kutoa hotuba.
Ya kwanza: Atakayeoga josho kamili, kama kuoga janaba, kisha akaenda katika msikiti wa Ijumaa katika saa ya kwanza, ni kama katoa sadaka ya ngamia.
Ya pili: Mwenye kwenda saa ya pili ni kama katoa sadaka ya ng'ombe.
Ya tatu: Yeyote atakayekwenda saa ya tatu ni kama ametoa sadaka kondoo dume mwenye pembe.
Ya nne: Mwenye kwenda katika saa ya nne ni kama ametoa sadaka kuku.
Ya tano: Mwenye kwenda saa tano, ni kama ametoa yai katika sadaka.
Anapotoka imamu kwenda kutoa hotuba; Malaika waliokaa milangoni huacha kuwaandikia thawabu wale wanaoingia msikitini mmoja mmoja, na huja kusikiliza ukumbusho na hotuba.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية الرومانية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Himizo la kuoga siku ya Ijumaa kabla ya kwenda kuswali.
  2. Fadhila za kuwahi swala ya Ijumaa kuanzia saa za mwanzo wa mchana.
  3. Himizo la kwenda mbio katika matendo mema.
  4. Malaika huhudhuria swala ya Ijumaa na kusikiliza hotuba.
  5. Malaika wako katika milango ya misikiti, wakiwaandikia wale wanaokuja, mmoja baada ya mwingine, wanapokuja kwa ajili ya Swala ya Ijumaa.
  6. Amesema bin Rajab: Kauli yake: “Mwenye kuoga siku ya Ijumaa kisha akaondoka” Inaashiria kuwa josho lililopendekezwa kwa siku ya Ijumaa linaanza kwa kuchomoza alfajiri, na mwisho wake ni muda wa kwenda katika swala ya Ijumaa.