عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:
«أَقْرَبُ مَا يَكُونُ الْعَبْدُ مِنْ رَبِّهِ وَهُوَ سَاجِدٌ، فَأَكْثِرُوا الدُّعَاءَ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 482]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Palipo karibu zaidi kwa mja na Mola wake ni pale anapokuwa kasujudu,Basi zidisheni dua".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 482]
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa mahala palipo karibu zaidi kwa mja na Mola wake ni pale anapokuwa kasujudu; Na hii ni kwa sababu mwenye kusali huweka kiungo bora na kitukufu kuliko vyote katika mwili wake juu ya Ardhi kwa kujinyenyekeza na kujidhalilisha na kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- anapokuwa kasujudu.
Na ameamrisha -Rehema na amani ziwe juu yake- kukithirisha dua katika sijida, yanakusanyika mambo mawili katika hilo, kujidhalilisha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa kauli na vitendo.