+ -

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«لَيْسَ مِنَّا مَنْ لَطَمَ الخُدُودَ، وَشَقَّ الجُيُوبَ، وَدَعَا بِدَعْوَى الجَاهِلِيَّةِ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1294]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abdallahi bin Masudi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Si miongoni mwetu atakayepiga mashavu, na akachana mifuko, na akaomboleza kwa maombolezo ya watu wa zama za ujinga".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1294]

Ufafanuzi

Amekataza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- na akatahadharisha kuhusu baadhi ya vitendo vya watu zama za ujinga akasema: Si miongoni mwetu:
La kwanza: Atakayepiga mashavu, na ametaja mashavu pekee kwa sababu ndio watu hufanya mara nyingi katika hilo, na vinginevyo kupiga sehemu zingine kunaingia ndani uso.
La pili: Kuchana uwazi wa nguo ili aingize kichwa kwa sababu ya huzuni kubwa.
La tatu: Akaomboleza kwa maombolezo ya za zama za ujinga kama kujiombea maangamivu na laana, na malalamiko, na makelele na mengineyo.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Thai Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الرومانية Luqadda Oromaha
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kemeo lililokuja katika hadithi hii linaonyesha kuwa matendo haya yote ni katika madhambi makubwa.
  2. Ulazima wa kuwa na subira katika msiba, na uharamu wa kuchukizwa na kadari za Mwenyezi Mungu zenye kuumiza, na kulidhihirisha hilo: Kwa kulia kwa malalamiko au makelele au kunyoa, au kuchana nguo au mengineyo.
  3. Uharamu wa kuwaiga watu wajinga kwa mambo yao ambayo sheria imeyathibitisha kwao.
  4. Hakuna tatizo kuhuzunika na kulia, kwani hili halipingani na subira juu ya makadirio ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, bali ni huruma aliyoiweka Mwenyezi Mungu katika nyoyo za ndugu wa karibu na vipenzi.
  5. Ni lazima kwa muislamu kuridhia maamuzi ya Mwenyezi Mungu, na asiporidhia basi kusubiri ni wajibu.