عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المؤْمنينَ رَضيَ اللهُ عنها قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي مَرَضِهِ الَّذِي لَمْ يَقُمْ مِنْهُ:
«لَعَنَ اللهُ الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى، اتَّخَذُوا قُبُورَ أَنْبِيَائِهِمْ مَسَاجِدَ» قَالَتْ: فَلَوْلَا ذَاكَ أُبْرِزَ قَبْرُهُ، غَيْرَ أَنَّهُ خُشِيَ أَنْ يُتَّخَذَ مَسْجِدًا.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 529]
المزيــد ...
Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa katika maradhi yake ambayo hakuweza kuamka tena:
"Amewalaani Mwenyezi Mungu Mayahudi na Wakristo, waliyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa mahali pa kusalia" Akasema: Na lau kama isingekuwa kauli hiyo basi lingenyanyuliwa kaburi lake, isipokuwa ilihofiwa kufanywa kuwa mahali pa kuswalia.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 529]
Anaeleza Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema akiwa katika maradhi yake ambayo yalikuwa makali na akafariki ndani yake: Mwenyezi Mungu aliwalaani Mayahudi na Wakristo, na aliwafukuza kutoka katika rehema yake; na hii ni kwa sababu wao waliyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa mahali pa kuswalia, na hii ni kwa kuyajengea au kuswali hapo au kwa kuyaelekea. Kisha akasema radhi za Allah ziwe juu yake: Na lau kama si katazo hilo na tahadhari hiyo kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na hofu ya Maswahaba kufanywa kaburi la Mtume rehema na amani ziwe juu yake kama walivyofanya Mayahudi na Wakristo kwa makaburi ya Manabii wao, basi lingedhihirishwa na kunyanyuliwa kaburi lake.