عَنْ عُبَادَةَ بْنِ الصَّامِتِ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«لَا صَلَاةَ لِمَنْ لَمْ يَقْرَأْ بِفَاتِحَةِ الكِتَابِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 756]
المزيــد ...
Kutoka kwa Ubaada bin Swaamit -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume -Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Hana swala yeyote ambaye hakusoma sura kifunguzi cha kitabu (suratul faatiha)".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 756]
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa sala haikubaliki isipokuwa kwa kusoma suratul Fatiha, nayo ni nguzo miongoni mwa nguzo za swala, katika kila rakaa.