عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«أَسْوَأُ النَّاسِ سَرَقَةً الَّذِي يَسْرِقُ صَلَاتَهُ» قَالَ: وَكَيْفَ يَسْرِقُ صَلَاتَهُ؟ قال: «لَا يُتِمُّ رُكُوعَهَا، وَلَا سُجُودَهَا».
[صحيح] - [رواه ابن حبان] - [صحيح ابن حبان: 1888]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Mwizi mbaya zaidi kuliko watu wote, ni yule anayeiba swala yake" Akasema: Ataiba vipi swala yake? Akasema: "Hatimizi rukuu zake wala sijida zake".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Ibnu Hibaan] - [صحيح ابن حبان - 1888]
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwizi mbaya zaidi kuliko wote ni yule anayeiba swala yake; na hii ni kwakuwa; kuchukua mali ya mtu mwingine huenda mtu akanufaika nayo duniani, tofauti na mwizi huyu, kwa sababu kaiba haki ya nafsi yake katika thawabu na malipo, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na vipi mtu anawezaiba kutoka katika swala yake? Akasema: Kwa kutotimiza rukuu zake wala sijida zake; na hii ni pale anapofanya haraka kutoka katika rukuu na sijida, hazileti katika namna ya ukamilifu.