عن ابن عباس رضي الله عنهما عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «أمِرْت أن أسْجُد على سَبْعَة أعَظُم على الجَبْهَة، وأشار بِيَده على أنْفِه واليَدَين والرُّكبَتَين، وأطْرَاف القَدَمين ولا نَكْفِتَ الثِّياب والشَّعر».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Nimeamrishwa nisujudu kwa viungo saba,paji la uso, na akaashiria kwa mkono wake katika pua yake, na mikono miwili na magoti mawili, na ncha za miguu miwili,na wala tusizikunje nguo na nywele".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Maana ya hadithi: "Nimeamrishwa nisujudu" Na katika riwaya nyingine "Tumeamrishwa": Na katika riwaya nyingine "Ameamrisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-; Na riwaya zote tatu ni za Imamu Bukhariy, na kanuni ya kisheria nikuwa: Alichoamrishwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- hicho ni amri kwake na kwa umma wake; "makusudio ya viungo saba": Yaani: nimeamrishwa nisujudu juu ya viungo saba, katika hadithi imetajwa mifupa; makusudio ya mifupa ni viungo vya kusujudia, kama ilivyokuja imetafsiriwa katika riwaya nyingine, kisha akavifafanua kwa kauli yake "Juu ya paji la uso" Yaani nimeamrishwa nisujudu kwa paji la uso, pamoja na pua kama inavyoonyesha kauli yake: "Na akaashiria katika pua yake", Yaani akaashiria katika pua yake ili aweke wazi kuwa hicho ni kiungo kimoja. "Na mikono miwili" Yaani na ndani ya viganja vyake, kama jinsi inavyokusudiwa hivyo kwa ujumla , "Na magoti mawili na ncha za miguu miwili" Yaani: Na nimeamrishwa nisujudu kwa magoti mawili na juu ya ncha za vidole vya miguu miwili, na katika hadithi ya Abii Humaidi As sa'idiy- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- katika kuelezea sifa ya swala kwa tamko: (Na akaelekea kwa vidole vya miguu yake kibla) Yaani: naye akiwa kasujudu. "Na tusikunje nguo na nywele" Maana yake: tusikusanye wala tusikunje nguo na nywele kwasababu ya kusambaa wakati wa kurukuu na kusujudu, bali tuliache jambo katika hali yake kama lilivyo, ili mtu aporomoke katika ardhi na asujudu kwa viungo vyote na nguo na nywele.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Ulazima wa kusujudu katika swala kwa viungo saba; kwasababu asili ya amri ni ulazima.
  2. Nikuwa haitoshelezi kusujudu kwa paji la uso bila pua na pua bila paji la uso; kwasababu Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- alipotaja paji la uso akaashiria katika pua.
  3. Ulazima wa kusujudu kwa viungo vyote, na wala havitoshi baadhi ya hivyo, na paji la uso aweke juu ya ardhi atakachokiweza.
  4. Uwazi wake nikuwa hakuna ulazima wa kufunua chochote katika viungo hivi, kwasababu neno kuvisujudia linakuwa kwa kuviweka bila kuvifunua, na hakuna utata wowote kuwa kufunua magoti mawili si wajibu, kwa kile kinachohofiwa ni katika kufunua uchi, hivyo hivyo miguu miwili kwasababu ya kufaa kuswali na khufu (viatu mfano wa soks).
  5. Ubaya wa kukunja nguo katika swala.
  6. Ni machukizo kufumua nywele na kuzifunga nyuma ya kisogo, sawa sawa akusudie kulifanya hilo kwaajili ya swala au awe alikua hivyo kabla ya swala na akafanya hivyo kwa lengo jingine na akaswali katika hali hiyo bila dharura.