عن أَبِي حَازِمِ بْن دِينَارٍ:
أَنَّ رِجَالًا أَتَوْا سَهْلَ بْنَ سَعْدٍ السَّاعِدِيَّ، وَقَدِ امْتَرَوْا فِي الْمِنْبَرِ مِمَّ عُودُهُ، فَسَأَلُوهُ عَنْ ذَلِكَ، فَقَالَ: وَاللهِ إِنِّي لَأَعْرِفُ مِمَّا هُوَ، وَلَقَدْ رَأَيْتُهُ أَوَّلَ يَوْمٍ وُضِعَ، وَأَوَّلَ يَوْمٍ جَلَسَ عَلَيْهِ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، أَرْسَلَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَى فُلَانَةَ -امْرَأَةٍ من الأنصار قَدْ سَمَّاهَا سَهْلٌ-: «مُرِي غُلَامَكِ النَّجَّارَ أَنْ يَعْمَلَ لِي أَعْوَادًا أَجْلِسُ عَلَيْهِنَّ إِذَا كَلَّمْتُ النَّاسَ»، فَأَمَرَتْهُ فَعَمِلَهَا مِنْ طَرْفَاءِ الْغَابَةِ، ثُمَّ جَاءَ بِهَا، فَأَرْسَلَتْ إِلَى رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَأَمَرَ بِهَا فَوُضِعَتْ هَاهُنَا، ثُمَّ رَأَيْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَلَّى عَلَيْهَا وَكَبَّرَ وَهُوَ عَلَيْهَا، ثُمَّ رَكَعَ وَهُوَ عَلَيْهَا، ثُمَّ نَزَلَ الْقَهْقَرَى، فَسَجَدَ فِي أَصْلِ الْمِنْبَرِ ثُمَّ عَادَ، فَلَمَّا فَرَغَ أَقْبَلَ عَلَى النَّاسِ فَقَالَ: «أَيُّهَا النَّاسُ، إِنَّمَا صَنَعْتُ هَذَا لِتَأْتَمُّوا وَلِتَعَلَّمُوا صَلَاتِي».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 917]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Hazim bin Dinari:
Anasimulia kuwa watu fulani walikuja kwa Sahli bin Sa'di As-saaidi, wakiwa wamepatwa na shaka kuhusu mimbari (ya Mtume) ilitengenezwa kwa mti gani, wakamuuliza kuhusu hilo, akasema: Wallahi mimi ninajua imetokana na mti gani, na niliiona tangu siku ya kwanza ilipowekwa, na siku ya kwanza kuikalia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, aliagiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa fulani -Mwanamke aliyekuwa mke wa mmoja kati ya Maanswari (Watu wa Madina) -Sahli alimtaja kwa jina lake-: "Muamrishe kijana wako seremala anitengenezee kibao niwe nakalia ninapo zungumza na watu", akamuamrisha akatengeneza kutokana na mti wa Twarfa (Mti mfano wa mkaratusi) hupatikani msituni, kisha akaileta, yule mama akaiagiza kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akaamrisha ikawekwa hapa, kisha nikamuona Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa juu yake na akatoa takbira (Allahu Akbaru) akiwa juu yake, kisha akarukuu akiwa ju yake, kisha akashuka kinyumenyume akasujudu mwishoni mwa mimbari, kisha akarudi, alipomaliza swala yake akawageukia watu kisha akasema: "Enyi watu! Bila shaka nimefanya hivi ili muige na mjifunze swala yangu".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 917]
Walikuja baadhi ya watu kwa mmoja kati ya Masahaba wakimuuliza kuhusu Mimbari ya Mtume aliyoitumia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ilitengenezwa kwa kitu gani? Na walikuwa wamekwisha bishana na kuzozana katika hilo, akawaeleza kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-aliagiza kwa mwanamke wa ki Answari alikuwa na mtumishi seremala, akamwambia: Mwamrishe kijana wako anitengenezee Mimbari nikalie wakati nikizungumza na watu, mama yule akakubali ombi hilo, na akamuamrisha kijana wake amtengeneze Mimbari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutokana na mti wa Twarfaa (Mti mfano wa mkaratusi), kijana alipomaliza kazi, yule mama aliaigiza kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Mtume akaamrisha iwekwe mahala pake msikitini, kisha akaswali Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa juu yake, na akatoa takbira akiwa juu yake, kisha akarukuu akiwa juu yake, kisha akashuka akiwa anatembea kwa nyuma bila ya kugeuka kutazama nyuma, akasujudu mwishoni mwa Mimbari, kisha akarudi, alipomaliza swala akawageukia watu, na akasema: Enyi watu!, Bila shaka nimefanya hivi ili muige na mjifunze swala yangu.