عن سالم بن أبي الجَعْدِ قال: قال رجل: ليتني صَلَّيتُ فاسترحْتُ، فكأنّهم عابُوا ذلك عليه، فقال: سمعتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يقول:
«يا بلالُ، أقِمِ الصَّلاةَ، أرِحْنا بها».

[صحيح] - [رواه أبو داود] - [سنن أبي داود: 4985]
المزيــد ...

Kutoka kwa Salim bin Abil Ja'di amesema: Mtu mmoja alisema: Laiti ningeswali nikastarehe, wakawa kana kwamba wamelitia dosari hilo, akasema: Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Ewe Bilali, simamisha swala, tupe raha kwayo".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Abu Daud] - [Sunanu Abii Daud - 4985]

Ufafanuzi

Akasema mtu mmoja katika Masahaba: Laiti ningeliswali nikastarehe, waliokuwa naye waka kana kwamba wamemuabisha kwa hilo, akasema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: Ewe Bilali! Nyanyua adhana na simamisha swala; ilitustarehe kwayo; na hii ni kwa sababu ndani yake kuna kuzungumza na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na raha ya roho na moyo.

Katika Faida za Hadithi

  1. Raha ya moyo iko ndani ya swala; kwani ndani yake kuna kuzungumza na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  2. Kemeo kwa mvivu katika ibada.
  3. Atakayetekeleza wajibu ulio juu yake, na akajiweka mbali na dhima, atapata raha kwa ibada hiyo na atahisi utulivu.
Kuonyesha Tarjama
Lugha: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Ziada (57)