عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال: (سَأَلتُ النبِيَّ صلى الله عليه وسلم : أَيُّ العَمَلِ أَحَبُّ إلى الله؟ قال: الصَّلاَةُ عَلَى وَقتِهَا. قلت: ثم أَيُّ؟ قال: بِرُّ الوَالِدَينِ. قلت: ثم أَيُّ؟ قال: الجِهَادُ في سَبِيلِ الله. قال: حَدَّثَنِي بِهِنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ولو اسْتَزَدْتُهُ لَزَادَنِي).
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdillahi bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: (Nilimuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ni amali ipi inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ni (kuiswali) swala kwa wakati wake. Nikasema: kisha nini? Akasema: Ni kuwatendea wema wazazi wawili. Nikasema: Kisha ipi? Akasema: Ni jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Akasema: Alinihadithia hayo Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- na lau ningetaka aniongeze zaidi basi angeniongeza).
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Alimuuliza bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuhusu mambo ya kumtii Mwenyezi Mungu, Ni yapi yanayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu? Kwani kila amali inapozidi kupendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu na malipo yake yanakuwa mengi zaidi. Akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akibainisha: Hakika inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kuiswali swala ya faradhi kwa wakati wake ambao sheria imeweka mpaka kwasababu ndani yake kuna kufanya haraka kwenda katika wito wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kutekeleza amri yake, na kutilia umuhimu wajibu huu mkubwa. Na katika shauku yake na mambo ya kheri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-, hakutosheka na hili, bali alimuuliza ngazi ya pili, miongoni mwa yale anayoyapenda Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: Ni kuwatendea wema wazazi wawili. Kwani la kwanza ni haki halisi ya Mwenyezi Mungu, na hili ni haki halisi ya wazazi wawili, na haki ya wazazi wawili inakuja baada ya haki ya Mwenyezi Mungu, bali yeye Mtukufu katika utukufu wake anaambatanisha haki yao na kuwatendea wema na kumpwekesha yeye katika maeneo mengi ndani ya Qur'ani tukufu, kwa haki walizonazo za msingi, ikiwa ni mbadala wa juhudi walizozitoa kuanzia kusababisha kuwepo kwako mpaka malezi yako, na kukulisha, na huruma yao na upole wao juu yako. Kisha yeye -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akamuomba ziada mtu asiyekuwa na ubahili, kuhusu ngazi inayofuata katika mlolongo wa amali hizi njema, akasema: Ni jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwani ndio kilele cha uislamu na ndio nguzo yake, ambayo uislamu hauwezi kusimama isipokuwa kwa hiyo, na kupitia nguzo hiyo linakuwa juu jina la Mwenyezi Mungu na inaenea dini yake. Na kwa kuiacha kwake -Na Mwenyezi Mungu atuepushe na hilo- ni kuubomoa uislamu, na ni kuporomoka kwa waislamu, na ni kutoweka kwa umoja wao, na kupokonywa kwa mamlaka yao, na kuondoka kwa utawala wao na dola yao. Nayo ni faradhi ya lazima kwa kila muislamu, ikiwa hatopigana, na akawa hakuizungumzisha nafsi yake kuhusu kupigana, basi atakuwa amekufa katika sehemu ya unafiki.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama