+ -

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«‌إِنَّ ‌أَثْقَلَ صَلَاةٍ عَلَى الْمُنَافِقِينَ صَلَاةُ الْعِشَاءِ وَصَلَاةُ الْفَجْرِ، وَلَوْ يَعْلَمُونَ مَا فِيهِمَا لَأَتَوْهُمَا وَلَوْ حَبْوًا، وَلَقَدْ هَمَمْتُ أَنْ آمُرَ بِالصَّلَاةِ فَتُقَامَ، ثُمَّ آمُرَ رَجُلًا فَيُصَلِّيَ بِالنَّاسِ، ثُمَّ أَنْطَلِقَ مَعِي بِرِجَالٍ مَعَهُمْ حُزَمٌ مِنْ حَطَبٍ إِلَى قَوْمٍ لَا يَشْهَدُونَ الصَّلَاةَ، فَأُحَرِّقَ عَلَيْهِمْ بُيُوتَهُمْ بِالنَّارِ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 651]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Hakika swala nzito zaidi kwa wanafiki ni swala ya Ishaa na swala ya Alfajiri, na lau kama wangejua (malipo) yaliyomo, basi wangeziendea hata kwa kutambaa, na nilipania niamrishe swala ikimiwe(kusimamishwa), kisha nimuamrishe mtu mmoja awasalishe watu, kisha niondoke pamoja na wanaume wakiwa wamebeba mizigo ya kuni tuelekee kwa watu ambao hawahudhurii swala, ili niwachome na moto wakiwa ndani ya majumba yao".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 651]

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu wanafiki na uvivu wao wa kuhudhuria swala, hasa hasa swala mbili, Ishaa na Alfajiri, nakuwa laiti wangelijua kiwango cha malipo na thawabu katika kuzihudhuria swala hizo pamoja na jamaa ya waislamu, basi wangeliziendea hata kwa kutambaa mfano wa kutambaa kwa mtoto kwa mikono na magoti.
.. Bila shaka aliazimia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aamrishe swala ikimiweisimamishwe), na amuweke mtu awasalishe watu badala yake, kisha aondoke akiwa pamoja na watu watakaombebea mizigo ya kuni kwenda kwa watu wasiohudhuria swala ya pamoja (Jamaa) ili awachome wakiwa ndani ya majumba yao; kwa sababu ya ubaya wa waliyoyafanya katika madhambi, -lakini hakufanya hivyo- kwa sababu ndani ya majumba yao kuna wanawake na watoto wasio na hatia, na wengineo miongoni mwa wenye udhuru, wasiokuwa na dhambi.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف Luqadda Asariga الأوكرانية الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Hatari ya kuchelewa swala ya pamoja msikitini.
  2. Wanafiki hawakukusudia katika ibada zao isipokuwa kujionyesha na kutaka kusikika, hawaji katika swala ila katika wakati ambao watu wanawaona.
  3. Malipo makubwa katika swala mbili, Ishaa na Alfajiri kwa jamaa, nakuwa swala hizo zinastahiki zaidi kuziendea hata kwa kutambaa.
  4. Kuhifadhi swala mbili, Ishaa na Alfajiri ni sababu ya kusalimika na unafiki, na kuto kuzihudhuria ni katika sifa za wanafiki.